Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA-HAKI

DRC: Wafungwa 11 wafariki dunia kutokana na uhaba wa dawa Kinshasa

Wafungwa 11 wamepoteza maisha katika gereza kubwa nchini DRC la Makala jijini Kinshasa, tangu kuanza kwa mwaka huu wa 2020. Ripoti zinasema kuwa, vifo hivyo vimesababishwa na uhaba wa chakula na dawa katika gereza hilo.

Gereza la Makala, Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambako wafungwa 11 wameripotiwa kufariki dunia kwa ukosefu wa dawa na chakula.
Gereza la Makala, Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambako wafungwa 11 wameripotiwa kufariki dunia kwa ukosefu wa dawa na chakula. AFP PHOTO / JUNIOR D. KANNAH
Matangazo ya kibiashara

Wafungwa watatu walipoteza maisha siku ya Jumatatu, baada ya kukosekana kwa dawa za kuwatibu na familia zao zilishindwa kuwasaidia.

Afisa wa juu katika gereza hilo ambaye hakutaka jina lake kutajwa amesema kuwa, hali imekuwa mbaya kwa sababu tangu mwezi Oktoba mwaka uliopita, serikali haijatoa fedha za kulisaidia gereza hilo kununua dawa na chakula.

Waziri Célestin Tunda Ya Kasende anayeshughulikia masuala ya wafungwa amekiri kuwa, kumekuwa na ucheleweshwaji wa kutuma dawa na chakula, lakini hali hiyo sasa imerekebishwa kuanzia siku ya Jumatatu wiki hii.

Gereza ka Makala ambalo lilijengwa na wakoloni wa Ubelgiji, kuwapokea wafungwa 1,500 kwa sasa lina wafungwa karibu 9,000 na kufanya gereza hilo kuwa msongamano mkubwa wa wafungwa, suala ambalo linatishia afya ya wafungwa hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.