Pata taarifa kuu
SUDAN-USALAMA-AJALI

Kumi na nane waangamia katika ajali ya ndege Sudan

Watoto wanne ni miongoni mwa watu 18 waliopoteza maisha nchini Sudan, baada ya ndege ya kijeshi iliyokuwa inawasafirisha abiria na misaada ya kibinadamu kuanguka Magahribi mwa jimbo la Darfur.

Nchi ya Sudan imeendelea kushuhudia ndege za kijeshi zikitumiwa, kuwasafirisha abiria na kusababisha ongezeko la ajali kama hizi.
Nchi ya Sudan imeendelea kushuhudia ndege za kijeshi zikitumiwa, kuwasafirisha abiria na kusababisha ongezeko la ajali kama hizi. , a estimé le ministre tchadien des Affaires étrangères Moussa Faki .
Matangazo ya kibiashara

Ripoti zinasema kuwa, ndege hiyo ilianguka dakika tano baada ya kuondoka katika uwanja wa ndehge wa El Geneina, eneo ambalo hivi karibuni lilishuhudia mapigano ya kikabila.

Wafanyakazi saba wa ndege hiyo, Majaji watatu na raia wa kawaida nane ndio waliokuwa ndani ya ndege hiyo na wote wameangamia.

Maafisa nchini humo wanasema wanaendelea na uchunguzi, kubaini chanzo cha ajali hiyo.

Nchi ya Sudan imeendelea kushuhudia ndege za kijeshi zikitumiwa, kuwasafirisha abiria na kusababisha ongezeko la ajali kama hizi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.