Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

Kadinali Fridolin Ambongo aonya kuhusu athari zinazoweza kutokea baada ya kuigawa DRC

Kiongozi wa kanisa katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kadinali Fridolin Ambongo, amesema mjadala wa baadhi ya wanasiasa kutaka kuigawa nchi hiyo vipande ni uhalisia na wananchi hawapaswi kuukubali.

Kiongozi wa kanisa katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kadinali Fridolin Ambongo.
Kiongozi wa kanisa katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Kadinali Fridolin Ambongo. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Kadinali Ambongo amesema haya baada ya hapo jana kukutana na sehemu ya wabunge wa jimbo la Kivu Kaskazini, ambapo amewaeleza kuwa matukio ya maeneo ya Beni, Ituri, Rutshuru na Minemwe jimboni Kivu Kusini yanauhusiano mkubwa na siasa za nchi hiyo.

Kiongozi huyo amewataka wanasiasa kutotumia majukwaa yao kueneza chuki na kuwagawa raia kwa misingi ya maeneo wanakotoka, akisema Congo inapaswa kuwa moja katika vita dhidi ya uasi.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeendelea kushuhudia matokeo mbalimbali, hasa ukosefu wa usalama Mashariki mwa nchi hiyo, hali ambayo inahusishwa kundi la waasi wa Uganda wa ADF.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.