Pata taarifa kuu
SUDANI-HAKI

Maafisa 27 wa idara ya ujasusi wahukumiwa adhabu ya kifo kwa kumuua mwandamanaji Sudan

Mahakama ya Sudan imewahukumu maafisai 27 wa idara ya ujasusi adhabu ya kifo, baada ya kupatikana na hatia ya kumtesa hadi kufa mmoja wa waandamanaji mapema mwaka huu.

Waandamanaji wakiandamana katika mitaa ya Khartoum Oktoba 21, 2019.
Waandamanaji wakiandamana katika mitaa ya Khartoum Oktoba 21, 2019. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah
Matangazo ya kibiashara

Hii ni hukumu ya kwanza ya adhabu ya kifo kwa maafisa wa vikosi vya Sudan kwa mauaji ya waandamanaji, mwaka mmoja zaidi baada ya kuanza kwa maandamano makubwa dhidi ya utawala wa Omar Hassan Al Bashir.

Watu wasiopungua 177 waliuawa na vikosi vya usalama na jeshi walipokuwa wakizima maandamano hayo kwa kutumia nguvu za kupita kiasi, hata wakati mwengine wakifanya ukandamizaji dhidi ya maandamano hayo, kwa mujibu wa shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Amnesty International. Kamati ya madaktari iliyo karibu na waandamanaji imebaini kwamba watu 250 waliauawa katika ukandamizaji huo dhidi ya waandamanaji.

Idara ya ujasusi ya Sudan (NISS) ilihusika pakubwa katika ukandamizaji huo, na mwezi Julai jeshi ambalo lilikuwa likishikilia utawala wakati huo liliisifu idara hiyo na kuita idara kuu ya Ujasusi.

Mamia ya waandamanaji wamekusanyika leo Jumatatu katika mahakama ya Omdurman, mji jirani na Khartoum, ambapo kesi ya maafisa 27 wa idara ya ujasusi imesikilizwa.

Walikuwa wamebebelea picha za Ahmed al-Kheir, mwalimu kutoka jimbo la Kassala mashariki mwa nchi, aliyeuawa na maafisa hao.

- "Adhabu inayofaa" -

"Damu ya shujaa haingemwagika bure", "Haki imetendeka", "hii ni adhabu inayofaa", waandamanaji hao wameimba baada ya kutangazwa kwa uamuzi huo.

Baadhi ya waandamanaji walikuwa wamekuja kwa basi kutoka Kassala, kilomita 800 kutoka mji mkuu, kuhudhuria kesi hiyo.

"Tumekuja kuuunga mkono familia ya mwenzetu," Ahmed Hassan ameliamia shirika la habari la AFP.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.