Pata taarifa kuu
BURKINA FASO-MAUAJI-USALAMA

Askari 11 wauawa katika shambulio jipya Burkina Faso

Wanajeshi kumi na moja wameuawa katika shambulio la kuvizia usiku wa Desemba 24 kuamika Jumatano Desemba 25 katika kijiji cha Hallalé, katika mkoa wa Soum. Wakati huo huo, ujumbe wa serikali ulizuru mji wa Arbinda baada ya shambulio ambalo liligharimu maisha ya raia 35 na askari saba.

Askari wa jeshi la Burkina Faso katika mazoezi ya kijeshi. (Picha ya kumbukumbu).
Askari wa jeshi la Burkina Faso katika mazoezi ya kijeshi. (Picha ya kumbukumbu). © ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Askari wa kambi ya Namissiguia ndi walilengwa na shambulio hilo jipya. Kulingana na vyanzo vyetu, kikosi hicho kilikuwa kimepewa majukumu ya kuzingira njia inayotumiwa na makundi ya watu wenye silaha. Askari wa kikosi hicho waliuawa katika shambulio hilo la kuvizia walipokuwa katika shughuli hiyo ya kulinda usalama. Shambulio hilo lilitokea usiku wa Jumanne Desemba 24 kuamkia Jumatano Desemba 25 katika kijiji cha Hallalé, karibu na wilaya ya Tongomayel.

"Tunasaka wahalifu katika eneo hili, baadhi ya askari wetu wameshambuliwa na makundi ya kigaidi yenye silaha," kimesema chanzo kingine. Wanajeshi kadhaa wamepoteza maisha. Hata hivyo, washambuliaji watano wameuawa, kulingana na taarifa zetu.

Shambulio hilo limetokea saa chache baada ya shambulio jingine lililolenga kikosi cha askari na raia katika eneo la Arbinda, katika mkoa huo Soum. Ujumbe mkubwa wa serikali uliojumuisha mawaziri sita, ikiwa ni pamoja na waziri wa ulinzi na waziri wa ardhi, walizuru eneo lililoshambuliwa na kutia moyo vikosi vya usalama na wakaazi wa eneo hilo. Wajumbe wa serikali pia waliwataka raia kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano na vikosi vya usalama katika mapambano dhidi ya ugaidi.

►Soma pia: Shambulio Burkina: Raia 35 wauawa, ikiwa ni pamoja wanawake wengi

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.