Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-SORO-SIASA-USALAMA

Guillaume Soro alaani 'utawala wa kiimla Cote d'Ivoire'

Washirika wa karibu 15 wa spika wa zamani wa Cote d'Ivoire Guillaume Soro, wamehamishiwa Maca, sehemu wanakozuiliwa wafungwa jijini Abidjan, baada ya kufikishwa mbele ya mwendesha mashtaka wa Jamhuri.

Guillaume Soro wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika makazi yake huko Abidjan, Februari 15, 2019.
Guillaume Soro wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika makazi yake huko Abidjan, Februari 15, 2019. © ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Guillaume Soro ambaye aliwahi kuwa waziri mkuu wa Cote d'Ivoire mwaka 2007 hadi 2012, kulingana na mkataba wa kisiasa wa Ouagadougou, amelaani hatua hiyo ya serikali, akibaini kwamba serikali inaungwa mkono na baadhi ya mataifa ya Ulaya.

Guillaume Soro amelaani hatua ya serikali ya Cote d'Ivoire kumkatalia kurejea nchini kujiandalia uchaguzi wa urais wa mwaka 2020.

Katika ujumbe uliyotumwa kwenye mtandao wa Facebook Jumanne hii jioni, Desemba 24, Guillaume Soro, amesema 'hatua hizo za serikali zinaonyesha utawala wa kiimla unaoendelea nchini Cote d'Ivoire.

Kwa upande wa ofisi ya rais, inakumbusha kwamba spika wa zamani wa Bunge la taifa hajakataliwa kurudi Cote d'Ivoire, lakini kwamba atakaponyaga ardhi ya Cote d'Ivoire atakamatwa mara moja.

Guillaume Kigbafori Soro anakabiliwa na waranti wa kimataifa uliotolewa na serikali ya Cote d;Ivoire kwa makosa ya utakatishaji fedha, kujaribu kuhujumu usalama wa taifa na kupitisha mlango wa nyuma feanka za CFA bilioni 15.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.