Pata taarifa kuu
DRC-RWANDA-USALAMA

Muzito: Vita na Rwanda ni lazima ili kuimarisha usalama Mashariki mwa DRC

Mratibu wa muungano wa vyama vya upinzani nchini DRC wa Lamuka, Adolphe Muzito, ametoa wito kwa viongozi wa nchi yake kutangaza vita dhidi ya Rwanda, ambayo anaituhumu kuhusika na mdororo wa usalama Mashariki mwa nchi hiyo.

Waziri mkuu wa zamani wa DRC, Adolphe Muzito, mnamo mwaka 2012.
Waziri mkuu wa zamani wa DRC, Adolphe Muzito, mnamo mwaka 2012. © AFP / Junior D. Kannah
Matangazo ya kibiashara

Adolphe Muzito aliyasema hayo Jumatatu Desemba 23 katika mji mkuu wa DRC, Kinshasa, wakati wa mkutano wake wa kwanza na waandishi wa habari kama mratibu wa muungano wa vyama vya upinzani wa Lamuka.

Hata hivyo pendekezo lake hilo halikuungwa mkono na viongozi wengine wa Lamuka.

Kwa upande wa Adolphe Muzito, mratibu wa Lamuka, amesema kuweka tayari kikosi cha kuingilia kati haraka cha MONUSCO, itakuwa njia mbadala ya suluhisho la kurejesha amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) ). Amependekeza kile ambacho ametaja kuwa ni suluhisho kudumu.

Kwa mujibu wa Bw Muzito, 'Ili kutatua hali hiyo, nchi inapaswa kujipanga kwa vita na Rwanda. Ikiwa tunataka kudhibiti Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, tunapaswa kuingia vitani na Rwanda. Kwa kuingia vitani, kunahitajika jeshi lilo imara, kunahitajika utawala wenye nguvu, na ufadhili mzuri [na] kuiteka Rwanda. Mwishowe, kuifanya Rwanda kuwa moja ya maeneo ya DRC '.

Mvutano ndani ya Lamuka

Wakati wa mkutano huo na waandishi wa habari uliodumu karibu saa mbili, Adolphe Muzito pia ameomba Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Maziwa Makuu (CEPGL) kuingilia kati mara kwa mara ili kuepusha migogoro kati ya wanachama wake. Kwa hivyo, kuingia vitani hakutakuwa lazima.

'Ninaposema kuingia vitani na Rwanda, ni hali ambayo kwa wakati fulani inaweza kuhitajika ikiwa kwa wakati huu mambo hayatabadilika. Vita sio jambo ambalo tunaweka mbele sana, ' ameendelea.

Lakini hoja hiyo ya Adolphe Muzito imeonekana kuwa haiungwi mkono na viongozi wote wa Lamuka. Moïse Katumbi na Jean-Pierre Bemba, baada ya tangazo hilo walitoa taarifa ya pamoja wakilaani kauli hiyo na kubaini kwamba hawaungi mkono pendekezo hilo, ambalo wamesema ni 'itikadi isiyofaa'.

Mvutano huu unatokea wakati Adolphe Muzito na viongozi wengine wa Lamuka wamepanga kuzuru Beni, kuonyesha mshikamano wao kwa wakaazi wa eneo hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.