Pata taarifa kuu
ALGERIA-BOUTEFLIKA-KIFO-JESHI

Mkuu wa Majeshi aliyeshinikiza kujiuzulu kwa Bouteflika afariki dunia

Mkuu wa majeshi nchini Algeria Ahmed Gaid Salah, ambaye alipata umaarufu mkubwa baada ya kumwambia rais wa zamani Abdelaziz Bouteflika ajiuzulu, amefariki dunia.

Aliyekuwa Mkuu wa majeshi nchini Algeria Ahmed Gaid Salah,wakati wa uhai wake tarehe 19 Desemba wakati wa kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo
Aliyekuwa Mkuu wa majeshi nchini Algeria Ahmed Gaid Salah,wakati wa uhai wake tarehe 19 Desemba wakati wa kuapishwa kwa rais mpya wa nchi hiyo REUTERS/Ramzi Boudina
Matangazo ya kibiashara

Jenerali Salah, mmoja wa wapiganaji wa zamani wa nchi hiyo wakati wa vita vya uhuru kati ya mwaka 1954 hadi 1962, dhidi ya Wafaransa, amefariki dunia baada ya kupata mshtuko wa moyo.

Baada ya kujiuzulu kwa Bouteflika mwezi Aprili, Jenerali Salah alichukua madaraka kwa muda katika kipindi cha mpito.

Serikali ya Algeria imetangaza siku tatu za maombolezo na tayari Jenerali Said Chengriha ametangazwa kuwa mkuu mpya wa Majeshi.

Pamoja na kukumbukwa kumshinikiza rais wa zamani Bouteflika kuachia madaraka, alishirilki pakubwa kuandaa Uchahizi wa urais uliofanyika mwezi huu, licha ya maandamano makubwa ya kupinga uchaguzi huo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.