Pata taarifa kuu
UGANDA-SUDANI-BASHIR-HAKI

Mahakama ya Uganda yatoa waranti dhidi ya Omar Hassan al-Bashir

Mahakama Kuu ya Uganda imetoa waranti wa kukamatwa dhidi ya aliyekuwa rais wa Sudani Omar Hassan al-Bashir, ambaye yuko gerezani, baada ya kutimuliwa madarakani kwa shinikizo la jeshi.

Rais wa Sudan Omar Hassan al-Bashir katika mahakama ya Khartoum, Septemba 28, 2019.
Rais wa Sudan Omar Hassan al-Bashir katika mahakama ya Khartoum, Septemba 28, 2019. REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Majaji wamebaini kwamba serikali ilishindwa kutekeleza majukumu yake kwa kukataa kumkamata rais wa Sudani aliyetimuliwa madarakani wakati alipokuja Kampala mwaka 2016 na 2017, wakati Mahakama ya Kimataifa ya makosa ya Uhalifu ilitaka kiongozi huyo wa zamani wa udani akamatwe kwa mauaji ya kimbari, uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu.

Uamuzi huu wa Mahakama unakja wakati Alhamisi wiki hii Sudani iliadhimisha mwaka mmoja tangu wimbi la malalamiko dhidi ya kupanda bei ya mkate na mafuta kugeuka miito kumtaka mtawala wa muda mrefu wa Sudan Omar Hassan al-Bashir ang'atuke.

Mapinduzi ya Sudan yaliwafanya watu wawe na matumaini makubwa.

Mashirika ya kiraia nchini Uganda yamepata ushindi dhidi ya dikteta huyo wa zamani Sudani. Mara mbili, mnamo mwaka wa 2016 na 2017, Rais huyo aliyetimuliwa madarakani aliingia na kuondoka nchini Uganda bila kuwa na hofu yoyote.

Uamuzi wa Mahakama Kuu umemridhisha wakili Nicholas Opiyo, ambaye alizindua utaratibu huo mnamo mwaka 2017 kwa niaba ya wakfu wa waathiriwa nchini Uganda. 'Uganda haiwezi kuwa hifadhi ya wahalifu au wale wanaosakwa na mahakama mbalimbali, hata kama mtu huyo atakuwa ni rais serikali au la. Hata kama Omar al-Bashir yuko gerezani, mashtaka dhidi yake bado yana nguvu. Kwa wakati wowote atakuwa tayari kujibu thuma zinazomkabili', amesema wakili Nicholas Opiyo.

Mwezi Mei, 2016, Omar Hassan al-Bashir alihudhuria sherehe ya kuapishwa rais Yuweri Museveni baada ya ushindi wake wa uchaguzi. Wakati huo rais wa Uganda alibaini kwamba majaji wa Mahakam ya Kimataifa ya Makosa ya Uhalifu "hawana uwezo wowote". Wanadiplomasia wa kutoka Ulaya, Marekani na Canada waliokuwa wakihudhuria sherehe hiyo waliondoka, ishara ya kupinga kauli hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.