Pata taarifa kuu
SUDA-SIASA-USALAMA

Mwaka mmoja wa maandamano yaliomuondoa madarakani Omar Hassan Al Bashir

Maandamano ya Sudan, yalianza Desemba 19, 2018, wakati serikali ilipandisha bei ya mkate.Tangu wakati huo, maandamano yaliendelea na kulikuwepo mapambano kati ya polisi wa kuzuia ghasia na waandamanaji.

Maandamano ya furaha huko Khartoum baada ya Omar el-Bashir kutimuliwa madarakani, Aprili 11, 2019.
Maandamano ya furaha huko Khartoum baada ya Omar el-Bashir kutimuliwa madarakani, Aprili 11, 2019. © REUTERS/Stringer
Matangazo ya kibiashara

Maandamano baadae yaligeuka na kuwa ya kutaka rais Omar Al-Bashir kuondoka madarakani.

Omar al-Bashir alikaa madarakani toka 1989.

Waziri wa Ulinzi wa Sudan Awad Mohamed Ahmed Auf alitangaza kuwa kiongozi wa muda mrefu Omar al-Bashir ameondolewa madarakani na anashikiliwa mahala penye usalama.

Akizungumza kupitia Televisheni ya Taifa ya Sudan waziri huyo alisema kutokana na hali hiyo alitangaza hali ya dharura ya miaka mitatu na amri ya kutotoka nje wakati wa usiku kwa muda wa mwezi mmoja.

Alisema kwamba baraza la mpito linaundwa na litabaki madarakani kwa miaka miwili.

Miezi kadhaa baadae viongozi wa kijeshi na wale wa muungano wa upinzani walitangaza kuundwa kwa baraza huru la uongozi ambalo litatawala kwa mpito katika kipindi cha miaka 3 kuelekea kupata serikali ya kiraia.

Baraza hilo lenye wajumbe 11, lilitangazwa na msemaji wa baraza la mpito la kijeshi ambalo limekuwa likitawala tangu kuangushwa kwa utawala wa Omar al-Bashir mwezi Aprili mwaka huu.

Wakati huu, mchakato wa kuundwa serikali ulianza nchini humo. Orodha ya wajumbe kumi na moja watakaoshiriki katika Baraza Kuu Tawala ilitangazwa kwenye televisheni na Chamseddine Kabbachi, msemaji wa Baraza la Jeshi la Mpito.

Iliafikiwa kwamba Baraza Kuu Tawala litaongozwa kwa kipindi cha miezi 21 na Jenerali Abdel Fattah al-Burhan, aliye kuwa mkuu wa Baraza la Jeshi la Mpito ambaye alichukua hatamu ya uongozi wa nchi baada ya rais Omar al-Bashir kutimuliwa madarakani mnamo mwezi Aprili baada ya miongo mitatu madarakani.

Kipindi cha mpito kuelekea utawala wa kiraia nchini Sudan, kufuatia mkataba wa kihistoria kati ya jeshi na viongozi wa maandamano, kilianza Jumatano Agosti 21 kwa kutawazwa kwa rais wa Baraza Kuu Tawala, Jenerali Abdel Fattah al-Burhan.

Baada ya siku kadhaa Abdallah Hamdok, 61, aliteuliwa kuwa Waziri Mkuu mpya wa Sudani, na alikula kiapo mbele ya rais wa Baraza Kuu Tawala.

Maandamano nchini Sudan yalianza mnamo Desemba 19, yalianzishwa kupinga kupanda kwa bei ya mkate katika miji ya pwani ya mto Nile, Atbera na Port Sudan, lakini baadae yalienea nchi nzima na lengo sasa likiwa ni kuipinga serikali.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.