Pata taarifa kuu
ALGERIA-SIASA-UCHAGUZI

Uchaguzi wa urais Algeria: Raia wamiminika mitaani kupinga uchaguzi

Baada ya takriban miezi kumi ya maandamano , wapiga kura milioni 24 nchini Algeria wametakiwa kupiga kura ili kumchagua mrithi wa rais wa zamani aliejiuzulu Abdelaziz Bouteflika. Raia wameingia mitaani kupinga kufanyika kwa uchaguzi huo.

Waandamanaji wakiimba nyimbo zinazopinga uchaguzi wa urais Desemba 12 Algiers.
Waandamanaji wakiimba nyimbo zinazopinga uchaguzi wa urais Desemba 12 Algiers. © REUTERS/Ramzi Boudina
Matangazo ya kibiashara

Wananchi wa Algeria wameendelea kuandamana katika miji mbalimbali nchini humo wakidai mageuzi kamili ya mfumo wa kisiasa nchini mwao na kupinga uchaguzi wa rais ambao unafanyika leo Alhamisi Desemba 12, 2019.

Hata hivyo uchaguzi huo unaoungwa mkono na jeshi, kwa mujibu wa vyanzo kadhaa kutoka kwa waandamanaji

Wakati huo huo, viongozi wamekuwa wakisema mara kwa mara kwamba uchaguzi nchini Algeria ndio jibu kwa matatizo yanayoikabili nchi hiyo kwa sasa. Uchaguzi utafanyika, vyanzo kadhaa kutoka serikalini vimebaini. Vituo vya kupigia kura vilitarajiwa funguliwa saa mbili asubuhi leo Alhamisi Disemba 12.

Wengi nchini algeria na nje ya nchi hiyo wanajiuliza kuhusu uchaguzi huo iwapo utafanyika kwa amani na usalama.

Baadhi ya mameya, kama vile katika mkoa wa Tizi Ozou katika Jimbo la Kabylie, wamesema hawako tayari kuandaa uchaguzi huo katika jimbo hilo. Pamoja na upinzani huo, viongozi wa mpito wa Algeria wamesema wako tayari kuandaa uchaguzi huo.

Wapiga kura milioni ishirini na nne wameorodheshwa kwenye daftari la wapiga kura na watu 500,000 watahusika na kusimamia uchaguzi katika vituo zaidi ya 60,000 vya kupigia kura nchini Algeria, mamlaka ya uchaguzi imetangaza.

Kwa siku kadhaa, kwenye vyombo vya habari vya serikali, viongozi wameendelea kutoa wito kwa wananchi 'kuitikiwa kwa kishindo uchaguzi huo'.

Mamlaka ya uchaguzi imethibitisha kwamba kiwango cha ushiriki kwa wananchi wa Algeria waishio ugenini kilifikia 20% Jumanne wiki hii saa saba mchana. Hii inamaanisha kuwa karibu watu 182,000, ambao wengi wao wameorodheshwa kwenye daftari la wapiga kura nchini Ufaransa, walijielekeza kwenye vituo vya kupigia kura.

Viongozi mbalimbali wametoa wito kwa wananchi, wakiwataka waandamanaji wasiwazuie wale wanaotaka kupiga kura.

Kuna karibu wagombea 22 walojiandikisha kwa uchaguzi wa urais na kwa mara ya kwanza hakuna mgombea kutoka chama tawala cha muda mrefu cha FNL .

Jeshi la taifa lenye ushawishi mkubwa katika siasa za Algeria halimuungi mkono mgombea yeyote katika juhudi za kuwahakikishia wananchi kwamba uchaguzi utakuwa huru na wa haki.

Lakini wengi kati ya wanaoandamana hawaamini kama msimamo huo utaleta mabadiliko yeyote.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.