Pata taarifa kuu
NIGER-SAHEL-USALAMA

Shambulio Niger: Nchi za Sahel zaendelea kukumbwa na mashambulizi mabaya

Mamia ya wapiganaji wa kijihadi wameshambulia kambi ya jeshi la Niger jirani na mpaka wa nchi ya Mali ambapo wanajeshi 71 wameripotiwa kuuawa, taarifa ya jeshi la nchi hiyo imethibitisha.

Askari wa jeshi la Niger wakipiga doria, mnamo Juni 2016 (picha ya kumbukumbu).
Askari wa jeshi la Niger wakipiga doria, mnamo Juni 2016 (picha ya kumbukumbu). © ISSOUF SANOGO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Shambulio la Jumanne ya wiki hii katika mkoa wa Tillaberi, ni baya zaidi kutekelezwa kulenga wanajeshi wa Niger tangu makundi ya kijihadi yaanze uasi nchini humo mwaka 2015.

Taarifa ya wizara ya ulinzi imesema wanajihadi waliokuwa wamejihami kwa bunduki na maroketi, wanaokadiriwa kufikia zaidi ya 100 na inaelezwa waliwashtukiza wanajeshi hao.

Shambulio hili linajiri huku vikosi vya nchi 5 za Sahel, vikiendelea kukumbana na changamoto za kifedha na uwezo wa kulinda maeneo ya mipaka.

Rais wa Burkina Faso, Rock Marc Kabore, ambaye nchi yake inashiriki katika operesheni za kijeshi dhidi ya makundi ya kijihadi, ametoa wito kwa wananchi wa ukanda huo kuungana na kuzuia vijana wao kujiunga na makundi hao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.