Pata taarifa kuu
MALI-UFARANSA-USALAMA-USHIRIKIANO

Sahel: Ufaransa yamwalika rasmi Rais wa Mali katika mkutano wa kilele wa Pau

Baada ya Niger, mjumbe maalum wa Ufaransa kwa Sahel, Christophe Bigot, alipokelewa kwa mazungumzo Jumanne (Desemba 10) na Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keita (IBK), ambaye alimkabidhi mwaliko rasmi kutoka kwa rais wa Ufaransa kuhudhuria mkutano wa Pau uliopangwa kufanyika Disemba 16.

Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta (IBK), kupitia Chirstophe Bigot, mjumbe maalum wa Ufaransa katika Ukanda wa Sahe,l amepokea barua rasmi ya mwaliko kutoka kwa Rais Macron (picha ya kumbukumbu).
Rais wa Mali Ibrahim Boubacar Keïta (IBK), kupitia Chirstophe Bigot, mjumbe maalum wa Ufaransa katika Ukanda wa Sahe,l amepokea barua rasmi ya mwaliko kutoka kwa Rais Macron (picha ya kumbukumbu). Don EMMERT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya Koulouba, makao makuu ya rais wa Mali iliyoko kwenye milima ya mji mkuu wa Bamako, imeiambia RFI kuwa imeridhika na mazungumzo na mjumbe huyo ambayo yalikwenda "vizuri", na kwamba ujumbe kutoka pande zote mbili ni mzuri.

Katika barua ya Emmanuel Macron kwa Rais IBK - ambayo RFI iliweza kupata nakala - mambo yako wazi: sio mwaliko wa kujieleza. Walakini, Bamako ilikasirishwa na kauli iliyotumiwa na Rais Macron mbele ya waandishi wa habari. "Lakini tunapaswa kusonga mbele na mshirika wetu, na pia rafiki yetu Ufaransa," amesema msaidizi wa Rais rais wa Mali.

Desemba 16 katika mji wa Ufaransa wa Pau "1+ 4" ndio watashiriki mkutano huo, ikimaanisha kila rais atakuwepo na Waziri wake wa Mambo ya nje, Waziri wa Ulinzi, Mkuu wa majeshi na Mkuu wa idara ya ujasusi.

Kulingana na taarifa tulionayo, marais wote wa nchi za G5 wamekubali kusiriki mkutano huo, kwa sasa, ispokuwa Rais wa Chad, Idriss Deby, kwa tarehe hiyo atampokea mgeni wa heshima.

"Marais wote watano wanatakiwa kuwa pamoja," kimesema chanzo kilicho karibu na faili hiyo. Katika mkutano ujao wa Pau, tarehe ya kutoa vifaa vya jeshi kwa nchi za G5 inaweza kutangazwa.

Kwa upande wake, Mali itazungumzia kuhusu mji wa Mali wa Kidal, ambao bado uko mikononi mwa waasi wa zamani. "Paris inakubaliana kabisa na hoja hiyo", chanzo kilicho karibu ya rais wa Mali kimesema.

Katika mkutano huo wa Pau kutazungumziwa pia mamlaka mapya ya kikosi cha Ufaransa cha Barkhane na yale ya kikosi Maalum cha Ulaya katika Ukanda wa Sahel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.