Pata taarifa kuu
ALGERIA-MAANDAMANO-SIASA-UCHAGUZI

Maandamano yaendelea kabla ya uchaguzi wa urais Algeria

Maandamano yanaendelea kushika kasiki nchini Algeria ikiwa zimesalia siku mbili kabla ya uchaguzi wa urais. Jumanne, Desemba 10, maandamano makubwa yalifanyika katika miji mbalimbali ya nchi hiyo, lakini polisi ilijaribu kuzuia maandamano hayo. Watu kadhaa wamekamatwa.

Waandamanaji waliandamana Jumanne (Desemba 10) huko Algiers, siku mbili kabla ya uchaguzi wa urais unaoendelea kupingwa.
Waandamanaji waliandamana Jumanne (Desemba 10) huko Algiers, siku mbili kabla ya uchaguzi wa urais unaoendelea kupingwa. © REUTERS/Ramzi Boudina
Matangazo ya kibiashara

Katika mji mkuu wa Algeria Algiers, watu wengi walishiriki maandamano ya kila wiki Jumanne wii hii, licha ya vikosi vya usalama kupelekwa katika maeneo mbalimbali ya mji. Katika maandamano hayo, waandamanaji, hususan wanafunzi, wamekuwa wakiimba kwamba hawatapiga kura na kwamba wanataka utawala wa kiraia sio wa kijeshi.

Maandamano yalifanyika katika majimbo 19. Katika Jimbo la Annaba, mashariki mwa nchi, wanafunzi kadhaa na walimu wamekamatwa. Katika mji wa Sidi Bel Abbes, watu kadhaa walijeruhiwa katika makabiliano na polisi.

Lakini mbali na maandamano ya wanafunzi, kwa siku kadhaa, maandamano pia hufanyika jioni, kuandamana kupinga kufanyika kwa uchaguzi. Siku ya Jumanne maandamano ya kupinga kufanyika kwa uchauzi yalifanyika katika mji wa Oran, magharibi mwa nchi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.