Pata taarifa kuu
MALI-SAHEL-USALAMA

Vikosi vya jeshi la Mali vyakabiliwa na changamoto nyingi

Katika wiki za hivi karibuni, Mashambulizi ya makundi ya kigaidi nchini Mali ymeongezeka. Jeshi la Mali limeendelea kupoteza katika mashambulizi hayo. Wengi wanahoji uwezo wa vikosi vya jeshi vya Mali kwa kutekeleza jukumu lake.

Fama ina askari 14,000 na imepoteza karibu askari 150 katika miezi miwili iliyopita.
Fama ina askari 14,000 na imepoteza karibu askari 150 katika miezi miwili iliyopita. © Agnes COUDURIER / AFP
Matangazo ya kibiashara

"Ninalitazama jeshi langu, ninaogopa," waziri wa ulinzi wa Mali, Dahirou Dembélé, alisema mbele ya Bunge wiki iliyopita. Siku chache kabla, jeshi la Mali (Fama) lilipoteza askari 43 katika shambulizi huko Tabankort, kaskazini mwa Mali.

Wabunge wengi walihoji tatizo linalosababisha jeshi la Mali kutofanya vizuri kwa kazi yake, waziri alijibu kuwa ni kutokana na "wakati".

"Mnamo mwaka 2012 jeshi letu liligawanyika," aliongeza Waziri Dahirou Dembélé.

"Tangu mwaka 2012, Fama wamepiga hatua," Marc André Boisvert, mwandishi, aliyeandika kitabu kuhusu maswala ya jeshi la Mali, amesema, huku akibaini kwamba "lakini haitoshi kwa jeshi hilo kufanya vizuri kwenye uwanja wa mapambano. "Hakuna jeshi linaweza kuwa imara ndani ya kipindi cha miaka michache," amebaini Marc André Boisvert.

"Kuna ukosefu wa utashi wa kisiasa," amesikitika mbunge wa upinzaji. "Utawala umeendelea kutumia jeshi kwa ufisadi wake, kumekuwa na kesi nyingi sana kuhusu ufisadi hapa nchini, ikiwa ni pamoja na kesi ya ya soksi zilizotozwa ushuru mwingi, kesi ya helikopta zilizonunuliwa lakini hazikuweza kufanya kazi, na kesi nyingine nyingi tu," amesem ambunge huyo wa upinzani.

Leo Fama ina askari 14,000 na imepoteza karibu askari 150 katika miezi miwili iliyopita.

Askari wetu hawana vifaa. Wanawake wa askari hawataki waume zao waende katika eneo la Kaskazini, kwa sababu wanahofia kuwa hawatarudi, Awa Kouyaté, mbunge mwengine amesema.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.