Pata taarifa kuu
UFARANSA-MALI-IS-USALAMA

Kundi la IS ladai kusababisha ajali ya helikopta mbili za Ufaransa Mali

Kundi la wanamgambo wa Kiislamu la Islamic State limetangaza kwa wapiganaji wake ndio walisababisha ajali ya helikopta mbili za Ufaransa, iliyogharimu maisha ya askari 13 wa nchi hiyo nchini Mali.

Helikopta ya jeshi aina ya NH90 ya kikosi cha jeshi la Ufaransa, Barkhane,  katika eneo la Ndaki, Mali, Julai 29, 2019.
Helikopta ya jeshi aina ya NH90 ya kikosi cha jeshi la Ufaransa, Barkhane, katika eneo la Ndaki, Mali, Julai 29, 2019. © REUTERS/Benoit Tessier
Matangazo ya kibiashara

Helikopta mbili za kijeshi za Ufaransa ziligongana Jumatatu, Novemba 25 wakati wa operesheni ya kijeshi ya usiku dhidi ya wanamgambo wa Kiislamu kusini mwa Mali.

Kwa mujibu wa jeshi la Ufaransa, askari wa kikosi cha masuala ya vita vinavyoendeshwa kwa helikopta waliombwa kutoa msaada dhidi ya maadui, katika eneo ambalo kikosi cha jeshi la Ufaransa, Barkhane, kinaendesha operesheni zake dhidi ya makundi yenye silaha, ikiwa ni pamoja na kundi la Islamic State katika Ukanda wa Grand Sahara (GSIM).

Katika taarifa iliyorushwa kwenye vituo vyake habari, kundi la Islamic State kimebaini kwamba wapiganaji wake waliendesha shambulio la kushtukiza dhidi ya msafara wa magari ya askari wa Ufaransa katika eneo la Menaka, na mapigano yaliibuka.

Helikopta iliyokuwa imebeba askari waliokuja kusaidia kikosi cha askari wa ardhini, ilijaribu kutua kwenye eneo la mapigano, lakini "askari wa IS walilazimisha ndege hiyo kupoteza mawasiliano baada ya kushambuliwa na hivyo kupoteza mawasiliano na kugongana na helikopta nyingine, ajali ambayo iligharimu maisha ya askari 13 wa Ufaransa, "imesema taarifa hiyo.

Katika madai haya, kundi hilo halijasema kwamba walikaribia helikopta hizo, wakati wangeweza kufanya hivyo.

Hata hivyo jeshi la Ufaransa limekanusha madai hayo ya kundi la Islamic State.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.