Pata taarifa kuu
UFARANSA-MALI-BARKHANE-USALAMA

Rambi rambi zaendelea kutolewa kufuatia vifo vya askari 13 wa Ufaransa nchini Mali

Viongozi mbalimbali duniani anaendelea kutuma rambi rambi ka serikali ya Ufaransa baada ya askari kumi na tatu wa Ufaransa wa kikosi cha Barkhane kufariki dunia katika ajali ya helikopta mbili Jumatatu usiku Kaskazini mwa Mali.

Askari saba kati ya kumi na tatu waliofariki dunia, walikuwa wa kitengo cha 5 cha masuala ya helikopta za kivita (5 RHC).
Askari saba kati ya kumi na tatu waliofariki dunia, walikuwa wa kitengo cha 5 cha masuala ya helikopta za kivita (5 RHC). © Marie Casadebaig/RFI
Matangazo ya kibiashara

Baadhi wameanza kutilia mashaka uwepo wa vikosi vya Ufaransa katika ukanda wa Sahel.

Nchini Ufaransa, viongozi wa juu zaidi wa kisiasa na katika jeshi - rais Emmanuel Macron, Waziri wa Jeshi  na Mkuu wa majeshi - wamekaribisha ujasiri na nia nzuri ya kujitolea kwa askari hao kumi na tatu waliofariki dunia katika ajali hiyo.

"Tuko imara, tumeungana, tumejidhatiti" amesema Florence Parly, Waziri wa Jeshi.

Kikosi cha askari wa Ufaransa katika ukanda wa Sahel, Barkhane, kwa sasa ni kikosi kikubwa zaidi kinachoendesha shughuli zake nje ya Ufaransa na kinaundwa na askari 4,500 ambao walitumwa katika ukand huo. Kikosi hiki kinaendesha opereheni zake katika Ukanda wa Sahel tangu mwaka 2014.

Baadhi ya wanasiasa nchini Ufaransa wamekosoa uwepo wa kikosi hicho katika Ukanda aw Sahel.

Kwa upande wa Jean-Luc Mélenchon wa chama cha France Insoumise, amesema uwepo wa kikosi cha Ufaransa katika Ukanda wa Sahel kwa muda wa miaka sita haukuzaa chochote: "Ni muhimu kwa raia wa Mali kuchukuwa uamuzi. Sio Ufaransa kuamua kinachotakiwa kufanyika nchini Mali. "

Chama cha mrengo wa kushoto kinaomba kuwepo mjadala kuhusu uwepo wa kikosi cha Ufaransa nchini Mali na katika Ukand mzima wa Sahel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.