Pata taarifa kuu
UFARANSA-MALI-USALAMA

Askari 13 wa Ufaransa wafariki dunia katika ajali ya helikopta mbili Mali

Ufaransa umewapoteza askari wake kumi na tatu waliofariki dunia katika ajali ya helikopta mbili Jumatatu usiku, Kaskazini mwa Mali. Helikopta mbili za kikosi cha jeshi la Ufaransa Barkhane ziligongana wakati wa operesheni ya kupambana dhidi ya makundi ya kigaidi katika eneo la mpaka na Niger na Burkina Faso.

Askari wa Ufaransa na Mali wakipiga doria pamoja katika mitaa ya Menaka, jimboni Liptako, Mali, Machi 21, 2019.
Askari wa Ufaransa na Mali wakipiga doria pamoja katika mitaa ya Menaka, jimboni Liptako, Mali, Machi 21, 2019. © Daphné BENOIT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ajali hiyo ilitokea katika mji wa Liptako Gourma, ambapo mapigano yanaendelea kurindima katika eneo hilo, linalojulikana kama lenye mipaka mitatu, kati ya Mali, Niger na Burkina Faso. Makundi mengi ya kigaidi yanaendesha harakati zao katika eneo hilo ambalo ni rahisi kwao kuvuka mpaka na kuingia katika moja ya nchi hizo tatu na hivyo kujumuika na wakaazi wa eneo hilo ambao wamejikita sana kwenye ufugaji.

Ni katika eneo hilo lenye mchanga, Mashariki mwa Gao, katika mji wa Indelimane, ambapo jeshi la Mali lilipata pigo kubwa mnamo Novemba 1 katika shambulio lililogharimu maisha ya askari wake zaidi ya hamsini. Mwezi mmoja kabla, watu wasiopungua 40 waliuawa katika mashambulio mawili dhidi yangome za jeshi katika miji ya Boulkessy na Mondoro, karibu na mpaka na Burkina Faso.

Ni mara ya kwanza tangu miaka kadhaa iliyopita jeshi la Mali kupoteza idadi kubwa ya askari wake kama hiyo. Tangu wakati huo, jeshi la Mali lilitangaza kujiondoa kenye ngome na hivyo kusababisha ukosefu wa usalama karibu na mpaka wa Niger na Burkina Faso, eneo ambalo makundi ya kigaidi yanaendelea kuhatarisha usalama.

Katika eneo hilo, askari wa kikosi cha jeshi la Ufaransa, Barkhane ndio wanaendesha operesheni kwa ushirikiano na kikosi cha kimataifa cha G5 Sahel.

Kwa mujibu wa vyanzo rasmi, askari wa Ufaransa wanaendesha mapigano na wanamgambo wa kundi la EIGS, kundi la Islamic State katika Ukanda wa Sahara, linaloongozwa na Abu Walid al-Sahrawi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.