Pata taarifa kuu

Mauaji Beni: Wakaazi wenye hasira wachoma moto majengo ya manispaa ya jiji

Hali ya sintofahamu imeripotiwa Jumatatu asubuhi wiki hii, baada ya taarifa ya mauaji mapya katika jimbo la Beni. Raia wenye hasira wamevamia majengo ya manispa ya jiji na kuchoma moto baadhi yao.

Uharibifu uliotokea wakati wa maandamano ya hivi karibuni Beni, DRC, Machi 2019.
Uharibifu uliotokea wakati wa maandamano ya hivi karibuni Beni, DRC, Machi 2019. © ALEXIS HUGUET / AFP
Matangazo ya kibiashara

Taarifa ya mauaji mapya imetolewa leo Jumatatu asubuhi. Watu wanane wameuawa usiku wa kuamkia leo katika eneo la Boikene. Baada ya taarifa hiyo, raia wenye hasira wamevamia majengo ya manispaa ya jiji la Beni na kuchoma moto baadhi yao. Tukio hilo limetokea saa tatu asubuhi.

Raia wameendelea kuandamana dhidi ya ukosefu wa usalama katika mji wa Beni na viunga vyake. Kundi la waasi wa Uganda, ADF, limeendelea kutekeleza mashambulizi ya hapa na pale katika maeneo hayo.

Hali ya wasiwasi imeripotiwa katika mji wa Beni, milio ya risasi imesikika karibu na kambi mbili za kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO.

Waandamanaji wameweza kuingia katika moja ya kambi ya Walinda Amani na kupora vifaa kabla ya polisi wa DRC kuingilia kati. Polisi inanyooshewa kidole cha lawama kwa kuwafyatulia risasi za chuma waandamanaji kwa lengo la kuwatawanya.

Ni vigumu kujua idadi ya vifo na majeruhi kwa sasa. Hata hivyo mashahidi wanasema watu kadhaa wamejeruhiwa kwa risasi.

Kwa upande mwingine, mwanaharakati wa vuguvugu la Lucha, Obadi Muhindo, alipigwa risasi na polisi Jumamosi wakati alipokuwa akilalamikia "uzembe" wa MONUSCO.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.