Pata taarifa kuu
COTE D'IVOIRE-ICC-SORO-BLE GOUDE-SIASA

Guillaume Soro na Charles Blé Goudé wakutana kwa mazungumzo Hague

Mkutano kati ya Charles Blé Goudé na Guillaume Soro ambao ulisubiriwa kwa hamu na gamu, umefanyika Jumapili hii, Novemba 24 mjini Hague, nchini Uswisi.

Guillaume Soro (kulia) na Charles Blé Goudé (kushoto) Gagnoa, Côte d'Ivoire Oktoba 2007.
Guillaume Soro (kulia) na Charles Blé Goudé (kushoto) Gagnoa, Côte d'Ivoire Oktoba 2007. KAMBOU SIA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Viongozi hao wawili wa kisiasa hawajakutana kwa mazungumzo tangu kuzuka kwa mzozo wa baada ya uchaguzi wa urais wa Novemba 2010 nchini Cote d'Ivoire.

Mkutano huo umefanyika kwa jitihada za Guillaume Soro, mgombea urais katika uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika mwezi Desemba 2020 na ambaye kwa miezi kadhaa amekuwa akijaribu kuhamasisha upinzani dhidi Rais Alassane Ouattara.

Wawili hao hawakuwka wazi mazungumzo yao yaliyodumu karibu saa mbili.

Guillaume Soro na Charles Blé Goudé "wameiomba serikali ya Abidjan" kupanga "mikutano itakayo wajumuisha wanasiasa katika ngazi ya taifa", kulingana na taarifa yao ya pamoja, ili "kuepuka sababu zilizoibua mzozo wa hivi karibuni ambao ulisababisha vifo vingi nchini Côte d'Ivoire".

Katika mahojiano ya hivi karibuni, Charles Blé Goudé alibaini kwamba hataunga mkono mgombea yoyote kwa sasa. Charles Blé Goudé yuko chini ya masharti aliyowekewa na Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ay Jinai (ICC), kufuatia kuachiliwa kwake huru. Hawezi kuondoka Hague ambapo anaendelea kuishi, kwa kusubiri uamuzi kuhusu kuachiliwa kwake pamoja na Laurent Gbagbo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.