Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

DRC kupata msaada wa dola milioni 600 kutoka Marekani

media Rais wa DR, Félix Tshisekedi, ambaye amekuwa akifanya ziara katika nchi za kigeni kuomba kuungwa mkono katika miradi yake ya maendeleo kwa DRC. Sumy Sadurni / AFP

Marekani imeahidi kutoa msaada wa dola milioni 600 kusaidia serikali ya DRC ifikapo mwaka 2022 kwa kuunga mkono miradi ya maendelea ya Rais Felix Tshisekedi aliyeshika madaraka tangu mwezi Januari mwaka huu.

Taarifa hii imetolewa Alhamisi wiki hii na Balozi wa Marekani nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo (DRC) Mike Hammer, jijini Kinshasa, ambaye amefahamisha kuwa serikali ya Marekani imeamua kumuunga mkono rais Tshisekedi katika azma ya kuleta mabadiliko, ndani ya taifa hilo kubwa na tajiri barani Afrika.

Hammer amesema fedha hizo zitasaidia kufanikisha shughuli za maendeleo zinazohusiana na elimu, ukuaji wa uchumi, afya, kupambana na rushwa na utawala bora, lakini pia kinga ya mazingira na hali kadhalika misaada ya kibinadamu.

"Misaada ya Marekani katika sekta hizi imekadiriwa kufikia dola bilioni 1.25 tangu 2015," imeongezea taarifa hiyo.

Hivi karibuni DRC na Marekani zilisaini Makubaliano kuinua sekta hizo, ambapo Marekani iliwakilishwa na Mkurugenzi wa USAID Paul Sabatine, huku DRC ikiwakilishwa na Waziri wa Ushirikiano wa Kimataifa Pepin-Guillaume Manjolo Buakila.

Msaada wa Marekani unakuja siku chache baada ya Ufaransa kwa upande wake ikitangaza kwamba inaiunga mkono serikali ya DRC katika mapambano dhidi ya ugonjwa hatari wa Ebola mashariki mwa nchi hiyo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana