Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Algeria yaendelea kukumbwa na maandamano ya usiku, watu kadhaa wakamatwa

media Mamia ya waandamanaji wamemiminika mitaani Alhamisi usiku katika maeneo mengi ya mji wa Algiers wakipinga uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Desemba 12. © REUTERS/Ramzi Boudina

Ikiwa imesalia wiki tatu kabla ya uchaguzi wa urais uliopangwa kufanyika Desemba 12, waandamanaji wameendelea kupinga kufanyika kwa uchaguzi huo katika mazingira yaliyopo hivi sasa.

Katika maandamano yaliyofanyika Alhamisi jioni wiki hii katika mji mkuu wa Algeria, Algiers, waandamanaji kadhaa wamekamatwa na polisi, wakati wa operesheni ya kuzima maandamano hayo.

Mamia ya watu wameingia mitaani wakipinga kufanyika kwa uchaguzi na mabadiliko ya mfumo katika uongozi wa serikali ya Algeria.

Siku ya Jumatano, watu kadhaa walikamatwa, kwa mujibu wa shirika linalotetea kuachiliwa huru kwa wafungwa.

Maandamano haya hufanyika kila Jumanne na kila Ijumaa kwa miezi kadhaa sasa.

Kwa upande wake shirika la kimataifa la kutetea haki za binadamu la Amnesty international limevishutumu vyombo vya usalama kwa kutumia nguvu kupita kiasi wakati wa kuwakamata waandamanaji ambapo inadaiwa watu 29 wanashikiliwa na polisi mjini Algiers.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana