Pata taarifa kuu
DRC-EU-BENI-USALAMA

Dkt Mukwege atoa wito kwa EU kusaidia kurejesha usalama Beni

Daktari bingwa anayewatibu wanawake waliobakwa nchini DRC na Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka 2018, Denis Mukwege, ametolea wito Umoja wa Ulaya na Ufaransa kuchukua hatua za kijeshi kumaliza mauaji ya raia wilayani Beni, Mashariki mwa nchi hiyo.

Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Denis Mukwege, akipokelewa na umati wa watu mjini Bukavu, Desemba 27, 2018.
Mshindi wa Tuzo ya Amani ya Nobel, Denis Mukwege, akipokelewa na umati wa watu mjini Bukavu, Desemba 27, 2018. Fredrik Lerneryd / AFP
Matangazo ya kibiashara

Takribani watu 60 wameuawa katika Mkoa wa Kivu Kaskazini tangu tarehe 30 mwezi Oktoba mwaka huu, lawama zikielekezwa kwa kundi la wapiganaji wa Kiislamu kutoka uganda ADF licha ya uwepo wa vikosi vya walinda amani wa Umoja wa Mataifa, MONUSCO na jeshi la Congo FARDC.

Watu wengine 21 wametajwa kuuawa Jumatano wiki hii katika mashambulizi mawili yanayodaiwa kutekelezwa na ADF wilayani Beni na mji jirani wa Oicha kwa mujibu wa radio ya umoja wa mataifa, Okapi.

Mukwege amesema ’’Tunatoa wito kwa Ufanransa na Umoja wa Ulaya kutuma wataalamu wa kijeshi hapa..chini ya sheria kifungu cha 7 cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa ili kulinda raia wa Beni dhidi ya magaidi...”.

Daktari Mukwege alishinda Tuzo ya Amani ya Nobel mwaka jana kutokana
na kazi aliyofanya kuokoa maisha ya waathirika wa ukatili wa kingono
katika eneo la Mashariki mwa DRC

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.