Pata taarifa kuu
NIGERIA-UCHUMI

Nigeria: Hatua ya kufungwa kwa mipaka inaweza kuendelea hadi mwisho wa mwezi wa Januari

Ni miezi mitatu tu tangu Nigeria iamue kufunga mipaka yake, ikibaini kwamba ni hatua ya kupambana dhidi ya biashara haramu na makundi ya wahalifu. Hali ambayo inaathiri uchumi wa nchi jirani, haswa uchumi wa Benin na Niger.

Malori mengi yamezuiliwa kwenye mpaka wa Nigeria kama hapa kwenye mpaka na Niger na Nigeria Oktoba 19, 2019.
Malori mengi yamezuiliwa kwenye mpaka wa Nigeria kama hapa kwenye mpaka na Niger na Nigeria Oktoba 19, 2019. © BOUREIMA HAMA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Mazungumzo ya kidiplomasia yamekuwa yakifanyika mara kwa mara kwa wiki kadhaa ili kusitisha hatua hiyo ya kufungwa kwa mipaka, ambayo inasababisha mdororo mkubwa wa uchumi kwa majirani wa Nigeria.

Wiki iliyopita, Waziri wa Fedha wa Nigeria alibaini kwamba mapato ya serikali yamepungua kwa karibu Faranga za CFA bilioni 40.

Rais wa Nigeria alizungumza mara kadhaa na wenzake wa Benin na Niger.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.