Pata taarifa kuu
CHAD-CAR-USALAMA

Chad: Kiongozi wa waasi Jamhuri ya Afrika ya Kati Abdoulaye Miskine akamatwa N'Djamena

Viongozi wa waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati akiwemo Jenerali Abdoulaye Miskine, mmoja wa watu muhimu katika masuala ya siasa na usalama nchini humo wamekamatwa nchini Chad. Jenerali Abdoulaye Miskine aliwasili N'Djamena Jumatatu jioni.

Jamhuri ya Afrika ya Kati: Waasi karibu na eneo la ukaguzi Damara, Januari 2013 (picha ya kumbukumbu).
Jamhuri ya Afrika ya Kati: Waasi karibu na eneo la ukaguzi Damara, Januari 2013 (picha ya kumbukumbu). © Photo AFP / Patrick Fort
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa vyanzo kutoka Chad, Aboulaye Miskine na viongozi wengine watatu wa kundi la waasi nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati waliingia nchini Chad wakipitia Tissi, mji wa Kusini-Mashariki unaopakana na Chad, Sudani na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Jenerali Abdoulaye Miskine na wenzake hawakusikilizwa. Ndio maana walipewa hifadhi kwenye majengo ya idara ya ujasusi ya Chad badala ya hoteli kama ilivyokuwa kawaida.

Suala la kuwepo kwa viongozi hawa wa waasi wa Jamhuri ya Afrika ya Kati nchini Chad limebua maswali. Wengi wanajiuliza iwapo wametafuta hifadhi baada ya kuzuka kwa mzozo mkubwa wa kikabila katika siku za hivi karibuni kaskazini mashariki mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati..

Katika mahojiano na Gazeti la kila wiki la Jeune Afrique wiki iliyopita, rais wa Chad alisema kwamba serikali yake - ambayo mara nyingi imekuwa ikituhumiwa kuchochea machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati - inatarajia kutoa msaada kwa jirani yake wa Kusini kwa kurejesha utulivu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.