Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 25/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Beni: Watu 21 wauawa na watoto kadhaa watekwa nyara na waasi wa ADF

media Askari wa Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (FARDC) wakisimama karibu na silaha kubwa ya kurusha roketi nyingi kwa wakati mmoja huko Matombo, kilomita 35 kaskazini mwa Beni, Kivu Kaskazini, Januari 13, 2018. © AFP

Watu ishirini na moja wameuawa, wengine wanne wamejeruhiwa na watoto kadhaa wametekwa nyara katika mashambulizi mawili ya ADF usiku wa Jumanne kuamkia Jumatano Novemba 20 katika mji wa Beni na wilaya ya vijijini ya Oicha, mji mkuu wa Beni, kwa mujibu wa Radio Okapi.

Mashirika ya raia yameripoti vifo saba katika mji wa Beni. Idadi hii imethibitishwa na vyanzo vingine vya usalama ambavyo vimesema kuwa askari wawili wa DRC, FARDC, pia wamejeruhiwa wakati wa mapigano.

Leo Jumatano, makundi ya vijana yameandamana katika mji wa Boikene, huku wakiweka vizuizi kwenye barabara kuu, wakiomba jeshi la DRC ( FARDC), polisi na kikosi cha Umoja aw Mataifa nchini humo (MONUSCO) kuwalindia raia usalama wao.

Pia usiku wa kuamkia leo Jumatano, waasi wa ADF walifanya shambulio jingine katika eneo la Mavete katika wilaya ya vijijini ya Oicha. Vyanzo vya usalama vimeripoti kuwa raia watatu wameuwa, lakini mashirika ya kiraia yametoa idadi ya watu 14 ambao wameuawa katika shambulio hilo.

Mashirika hayo ya kiraia yanabaini kwamba yametahadharisha kuwa waasi wa ADF wamepenya na kuingia katika maeneo kadhaa ya mji wa Beni wakati jeshi la FARDC lilikuwa likiendesha mashambulizi dhidi ya kundi hilo.

Shambulio hili ni la kwanza la ADF katika mji wa Beni tangu Oktoba mwaka wa 2018.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana