Pata taarifa kuu
MALI-G5 SAHEL-USALAMA

Wanajiahdi 24 wauawa katika operesheni ya jeshi la G5 Sahel

Jeshi la Ufaransa linasema washukiwa 24 wa kijihadi wameuawa nchini Mali na Burkina Faso baada ya kushambuliwa na kikosi cha jeshi la G5 Sahel.

Kikosi cha G5 Sahel kutoka Mali, wakipiga doria Novemba 2017 karibu na mpaka na Burkina Faso.
Kikosi cha G5 Sahel kutoka Mali, wakipiga doria Novemba 2017 karibu na mpaka na Burkina Faso. Daphné BENOIT / AFP
Matangazo ya kibiashara

Ripoti za kijeshi zinasema kuwa kikosi cha G 5 Sahel kilitekeleza mashambulizi ya kushtukiza katika mpaka wa Mali na Burkina Faso.

Pamoja na mauaji hayo, simu zaidi ya 100 na silaha zilikamatwa wakati wa operesheni hiyo kwa kipindi cha wiki mbili zilizopita.

Jeshi hilo linasema kuwa, magaidi waliouuawa wametambuliwa.

Taarifa hii imekuja, wakati huu mkutano wa amani uliofanyika jijini Dakar nchini Senegal, kujadiliana kuhusu namna ya kupambana na makundi ya kijihadi katika eneo la Sahel.

Miezi ya hivi karibuni, magaidi hao wamekuwa wakiwalenga wanajeshi wa Mali na Burkina Faso na kusababisha utovu wa usalama katika nchi hizo mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.