Tanzania yaandelea kuwasaka watu waliohusika na shambulizi lililoua watu sita
Jeshi la Polisi na vyombo vingine vya usalama nchini Tanzania, vinaendelea kufanya uchunguzi ili wahusika wa shambulizi lililosababisha mauaji ya watu sita wanakamatwa na kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria.
Imechapishwa:
Watanzania sita waliuawa kwa kupigwa risasi na wengine saba kujeruhiwa katika shambulio lililofanywa na washambuliaji wasiojulikana katika kijiji kinachopakana na mkoa mmoja nchini Msumbiji unaojulikana kwa shughuli za kijihadi.
Mkurugenzi wa Upelelezi wa makosa ya jinai nichi Tanzania, Robert Boaz, amesema wanaliofanya shambulizi hilo walikimbilia msumbiji na bado wanawatafuta
Kwa karibu miaka miwili, wanajihadi wamefanya mshambulizi kadhaa katika mkoa wa Cabo Delgado nchini Msumbiji, unaopakana na Tanzania, na kuwauwa raia wasiopungua 300 na kusabaisha makumi kwa maelfu ya watu kukimbia makazi yao nchini Msumbiji.