Pata taarifa kuu
KENYA-SOMALIA-USHIRIKIANO

Kenya na Somalia zakubaliana kurejesha uhusiano wao wa awali

Kenya na Somalia, zimekubaliana kurejesha ushirikiano wa awali wa kidiplomasia na kuruhusu raia wa nchi hizo jirani kuvuka mpaka bila vikwazo. Hii inakuja, baada ya mazungumzo kati ya rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Mohamed Abdullahi Farmajo.

Uhuru Kenyatta na Mohamed Abdullahi Farmajo Nairobi, Novemba 14, 2019.
Uhuru Kenyatta na Mohamed Abdullahi Farmajo Nairobi, Novemba 14, 2019. © State House Kenya Kenya
Matangazo ya kibiashara

Uhusiano kati ya Mogadishu na Nairobi katika miezi kadhaa iliyopita, umeonekana kuwa baridi, baada ya Somalia kuishtaki Kenya katika Mahakama ya Kimataifa kuhusu mzozo wa mpaka wa Bahari kunakopatikana hifadhi ya mafuta.

Katika mkutano wao na waandishi na habari marais hao wawili wameonyesha mshikamano wao kwa kuwaambia waandishi wa habari kwamba Kenya na Somalia ni nchi jirani na ndugu na kubaini kwamba nchi hizo zimeamua kuweka kando tofauti zao na kurejesha uhusiano wao wa awali.

Baada ya mazungumzo yaliyodumu saa kadhaa, Uhuru Kenyatta na Mohamed Abdullahi Farmajo kwanza walionyesha mshikamano wao na kupeana mikono ishara kwamba nchi hizi ni rafiki na ndugu.

Lakini katika taarifa zao kwa waandishi wa habari, wote hawakuweka wazi tofauti zinazokumba nchi hizi mbilizi, wakati tofauti zao zinahusu maswala mengi.

Hii ni kama ishara ya nia njema, Wakenya na Wasomali watapewa visa wanapowasili nchi mojawapo kati ya hizo mbili, na safari za ndege za moja kwa moja kati ya Mogadishu na Nairobi zitaanza ndani ya kipindi cha wiki moja, amesema rais wa Kenya Uhuru Kenyatta.

Kwa upande wa mzozo wa baharini ambao utaamuliwa mwaka ujao na Mahakama ya Kimataifa ya Haki, marais hao hawakuzungumzia lolote. Farmajo ameikaribisha Kenya kwa ushiriki wake katika kikosi cha Umoja wa Afrika AMISOM, na kwa ukarimu wa Kenya kwa wakimbizi wa Kisomali. Na amesema "ana imani" kwamba mzozo huu "utatatuliwa kwa njia inayokubaliwa ambayo haitaathiri uhusiano wa nchi hizi mbili," akipendekeza mazungumzo ya moja kwa moja.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.