Pata taarifa kuu
ETHIOPIA-SIASA-HAKI

Ethiopia: Watu 68 washtakiwa kwa Jaribio la mapinduzi Amhara

Uchunguzi wa mauaji ya kisiasa mwishoni mwa mwezi Juni umekwisha, Waziri wa Sheria wa Ethiopia amesema. Mwendesha Mkuu Berhanu Tsegayé amebani kwamba tukio lililotokea Juni 22 ilikuwa ni jaribio la mapinduzi.

Mji wa Lalibela, katika Jimbo la Amhara, Kaskazini mwa Ethiopia, Februari 2, 2019 (picha kumbukumbu).
Mji wa Lalibela, katika Jimbo la Amhara, Kaskazini mwa Ethiopia, Februari 2, 2019 (picha kumbukumbu). © REUTERS/Thomas Mukoya
Matangazo ya kibiashara

Juni 22, rais wa Jimbo la Amhara aliuawa pamoja na viongozi wengine waandamizi wawili. Saa chache baadaye, Mkuu wa Jeshi la Ethiopia pia aliuawa Addis Ababa, baada ya kupigwa risasi na mmoja wa walinzi wake. Baada ya zaidi ya miezi mitano ya uchunguzi, viongozi wa Ethiopia wanadai kwamba Naibu Mkuu wa jeshi ndiye alikuwa anatarajiwa kuuawa.

Kwa mujibu wa Mwendesha mashitaka Mkuu, watu 110 walipewa mafunzo maalum kwa kuandaa mashambulizi haya. Berhanu Tsegayé amesema kuwa watu hao ni kutoka Jimbo la Amhara lakini pia kutoka mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, na sehemu za kusini au magharibi mwa nchi.

Polisi imekamata silaha, simu za mkononi, sarafu za ndani na nje na magari. Akaunti 22 za benki zimefungwa. Kwa jumla, watu 78 watashitakiwa mwishoni mwa juma kwa mujibu wa televisheni ya serikali Fana.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.