Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-UCHUMI

Noti mpya za Dola kutolewa kwa mara ya kwanza ndani ya kipindi cha miaka 10 Zimbabwe

Wananchi wa Zimbabwe wanaendelea kufurika katika Benki mbalimbali nchini humo,wakiwa na matumaini ya kupokea noti za kwanza za nchi hiyo ya Dola, ambayo inatolewa kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2009.

Dola milioni 200 za Zimbabwe mfomo wa noti uliotolewa mwaka 2016.
Dola milioni 200 za Zimbabwe mfomo wa noti uliotolewa mwaka 2016. Reuters/Philimon Bulawayo
Matangazo ya kibiashara

Noti hizo ziliondolewa karibu miaka 10 iliyopita, baada ya kuonekana kutokuwa na thamani na kusababisha bidhaa nchini humo kupanda maradufu.

Benki kuu nchini humo inatumai kuwa noti hizi mpya, zitasaidia kuongeza kiwango cha fedha kilichopo katika mikono ya watu na kusaidia kuinua uchumi wa nchi hiyo.

Noti za Dola mbili na tano ndizo zinazotolewa na tayari Benki Kuu imekanusha taarifa kuwa, inalenga kuchapisha kiwango kikubwa cha noti hizo, suala ambalo huenda likadimiza zaidi uchumi wa nchi hiyo.

Uchumi wa Zimbabwe umeendelea kuyumba kutokana na vikwazo ilivyowekewa na mataifa ya Magharibi tangu utawala wa rais wa zamani, hayati Robert Mugabe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.