Pata taarifa kuu
DRC-KANISA-SIASA-USALAMA

Kanisa Katoliki DRC kuanza kuchunguza sughuli za serikali

Askofu Mkuu wa kanisa Katoliki nchini DRC, Fridolin Ambongo Besungu, amejitokeza hadharani mbele ya vyombo vya habari jijini Kinshasa na kusema kuwa anataka kuchukua jukumu lake la utume katika kufuatilia kwa ukaribu masuala yote yanayofanyika nchini DRC.

Kardinali Fridolin Ambongo.
Kardinali Fridolin Ambongo. REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii inakuja miezi kadhaa baada ya kuteuliwa na kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis kama Kardinali.

Kardinali Fridolin Ambongo amezungumzia masuala mbalimbali ikiwemo mpango wa elimu ya bure iliyoamuliwa na Rais Felix Tshisekedi.

Amewataka wanasiasa wa muungano wa FCC unaoungwa mkono na rais wa zamani Jospeh Kabila na wale wa CACH kuwaonya wafuasi wao kudumisha amani.

Kiongozi huyo wa kanisa katoliki nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo Fridolin Ambongo amebaini kuwa kumekuwa na "ishara nzuri", zinazoleta matumaini katika kipindi cha miezi kumi ya utawala mpya katika nchi hiyo.

Fridolin Ambongo aliteuliwa na kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis kama Kardinali miezi kadhaa iliyopita.
Fridolin Ambongo aliteuliwa na kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis kama Kardinali miezi kadhaa iliyopita. Tiziana FABI / AFP
Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.