Pata taarifa kuu
GUINEA-UCHAGUZI-SIASA

Uchaguzi wa wabunge kufanyika Februari 16, 2020 Guinea

Tume ya Uchaguzi nchini Guinea, imetangaza kuwa Uchaguzi wa wabunge ambao umekuwa ukiahirishwa mara kwa mara sasa utafanyika mwezu Februari mwaka 2020.

Raia wakiandamana katika mji muu wa Guinea, Conakry, Oktoba 24, 2019
Raia wakiandamana katika mji muu wa Guinea, Conakry, Oktoba 24, 2019 CELLOU BINANI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Tangazo la tume ya uchaguzi linakuja, wakati huu maandamano yakiendelea kwa wiki kadhaa sasa, kupinga uwezekano wa rais Alpha Conde kuwania tena urais kwa muhula mwingne.

Mwenyekiti wa tume hiyo Amadou Salif Kebe amesema kuwa uchaguzi huo utafanyika tarehe 16 mwezi Februari mwaka ujao.

Hata hivyo, bado kuna wasiwasi iwapo uchaguzi huo utafanyika kwa sababu umekuwa ukipangwa na kuahirishwa mara kwa mara.

Mwezi Septemba, tume ya uchaguzi ilikuwa imepanga kufanyika kwa uchaguzi huu tarehe 28 mwezi Desemba lakini hilo halijafanyika.

Muda wa bunge lililopo ulimalizika mwaka 2018, lakini mvutano kati ya wanasiasa wa chama tawala na upinzami, umeendelea kuwa chanzo cha kutofanyika kwa uchaguzi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.