Pata taarifa kuu
DRC-SIASA-USALAMA

DRC: Mvutano mpya waibuka ndani ya muungano wa vyama viwili madarakani

Hali ya sintofahamu imeukumba ndani ya muungano unaojumuisha vyama viwili madarakani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, kile kinachomuunga mkono rais wa zamani na kile kinachomuunga mkono rais wa sasa.

Joseph Kabila na Felix Tshisekedi katika sherehe ya kuapishwa rais mpya wa DRC, Kinshasa Januari 24, 2019.
Joseph Kabila na Felix Tshisekedi katika sherehe ya kuapishwa rais mpya wa DRC, Kinshasa Januari 24, 2019. REUTERS/ Olivia Acland
Matangazo ya kibiashara

Wafuasi wa vyama hivyo wamekuwa wameendelea kukabiliana katika maeneo mbalimbali ya nchi hiyo. Katika miji ya Kinshasa na Lualaba, kupitia mitandao ya kijamii, wafuasi wa kambi hizo mbili wamendelea, kila upande, kuonyesha vitendo vya kiuhasama dhidi ya upande mwingine, na hivyo kuweka mashakani picha ya muungano kati ya kambi hizo mbili tawala.

Mabango makubwa ambayo yalikuwa na picha ya rais wa zamani Joseph Kabila, ambayo yaliwekwa kwa minajili ya mkutano wa hadhara uliopangwa kufanyika Desemba 14mjini Kinshasa, yameharibiwa karibu na makao makuu ya bunge la kitaifa, katikati mwa mji mkuu wa nchi hiyo.

Mwishoni mwa wiki hii iliopita, kilomita zaidi ya 2000, kutoka Kinshasa, katika mji wa Kolwezi, katika mkoa wa Lualaba, wafuasi wa rais wa zamani wa DRC, Josepha Kabila, kutokana na hatua ya wafuasi wa Felix Tshisekedi mjini Kinshasa, walichoma moto picha za rais wa sasa Felix Tshisekedi.

Chama cha UDPS kimelaumu viongozi wa mkoa wa Lualaba, kuona rais anadhalilishwa kwa picha zake kuchomwa hadharani.

Jean-Marc Kabund, makamu wa spika wa Bunge la Taifa ameandika kwenye ujumbe kwenye ukurasa wake wa twitter akipendekeza kusitishwa mazungumzo yote kati ya muungano wa Cach wa Félix Tshisekedi na FCC ya Joseph Kabila hadi pale wahusika wote wa vitendo hivyo watajulikana na wafikishwe mbele ya vyombo vya sheria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.