Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

ICC: Kiongozi wa zamani wa kivita DRC Bosco Ntaganda ahukumiwa kifungo cha miaka 30 jela

media Bosco Ntaganda wakati wa ufunguzi wa kesi yake mbele ya ICC Septemba 2, 2015. © REUTERS/Michael Kooren

Majaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Makosa ya Jinai (ICC) wamemhukumu mbambe wa zamani wa kivita nchini DRC Bosco Ntaganda kifungo cha miaka 30 jela.

Kiongozi huyo wa zamani wa kivita alipatikana na hatia ya uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita Julai 8, 2019.

Miaka thelathini gerezani: hii ndio hukumu ambayo Bosco Ntaganda amehukumiwa. Kiongozi wa zamani wa tawi la kijeshi la kundi la waasi la wa UPC la Thomas Lubanga, moja ya makundi ya wanamgambo yaliyoedesha uhalifu wake mashariki mwa DRC, mnamo mwaka 2002 na 2003, alipatikana na hatia Julai 8 ya mashambulio dhidi ya raia, mauaji, ubakaji, utumwa wa kingono, mateso, kuwatumikisha watoto kama wanajeshi na uporaji, uhalifu uliotajwa kama uhalifu dhidi ya binadamu na uhalifu wa kivita uliofanywa chini ya maagizo yake.

Ntaganda ambaye anajulikana kwa jina la "Terminator", yaani mmaliziaji, kwa sababu ya tabia yake ukatili, ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini DRC ulibaini, yeye mwenyewe alishiriki katika uhalifu huo, haswa kwa kumuua Padri Boniface Bwanalonga, Padri maarufu katika jamii ya Walendu.

Mwezi Julai , majaji watatu walimpata Ntaganda na hatia ya makosa yote 18 ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu uliofanyika katika jimbo lenye utajiri wa madini lililoko mashariki wa DRC la Ituri kati ya mwaka 2002 na 2003.

Ntaganda alikuwa "kiongozi muhimu " ambaye alitoa amri ya "kuwalenga na kuwauwa raia" jaji Robert Fremr alisema katika hukumu yake.

Hukumu dhidi yake ni ya muda mrefu kuwahi kutolewa katika historia ya mahakama ya ICC .

Ntaganda alikuwa ni mtu wa kwanza kupatikana na hatia ya utumwa wa ngono na mahakama ya ICC kwa kwa ujumla ni mtu wa nne ambaye mahakama hiyo imempata na hatia tangu ilipoundwa mwaka 2002.

Ntaganda ambaye alizaliwa nchini Rwanda mwenye umri wa miaka 46-muasi wa zamani amekuwa akihusika na mizozo mbali mbali ya kivita nchini Rwanda na Jamuhuri ya Kidemokrasi ya Congo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana