Pata taarifa kuu
TUNISIA-ELIMU-MGOMO

Wanafunzi waendelea na mgomo Tunisia, wana wasiwasi kuhusu uhuru wa kujieleza

Wanafunzi wa kitivo cha Utabibu katika Chuko Kikuu cha Tunis,na vyuo vikuu nchini kote Tunisia wanaendelea na mgomo walioanza tangu Jumatatu wiki.

Moja ya sehemu ya Chuo Kikuu cha Tiba cha Tunis, mnamo 2018.
Moja ya sehemu ya Chuo Kikuu cha Tiba cha Tunis, mnamo 2018. © Houssem Abida/wikipedia
Matangazo ya kibiashara

Wanafunzi hao wanatarajia kuandamana kupinga hatua ya malaka ya kumfukuza kwa miezi minne mwanafunzi wa kitivo cha Utabibu, aliyekosoa urasibu mbaya unaoripotiwa katika chuo kikuu cha Tunis.

Mwanafunzi huyo aliandika kwenye akaunti yake ya Facebook maoni mawili yanayokosoa hatua ya kufungwa kwa maktaba ya chuo kikuu. Ni jambo la kushangaza, aliandika.

Kwa kugoma Jumatatu baada ya kufukuzwa wa mwanafunzi hyo, wanafunzi walitaka kukemea "tabia mbaya ya kuadhibu" ambayo inatawala katika vyuo vikuu vya Tunisia.

Wanaogopa kurudi kwa tabia ya kukandamiza uhuru wa kujieleza. Kwa mujibu wa wanafunz hao, kesi za adhabu za halmashauri za nidhamu za vyuo vikuu zimeongezeka.

Katika taarifa, Jumuiya ya wanafunzi wa vyuo vikuu Tunis,UGET, imeonyesha uungwaji wake mkono kwa Wajih Thakkar, na kuomba aweze kurudi kuendelea na visomo katika chuo kikuu: Jumuiya hiyo ya wanafunzi, imebaini kwamba hatua ya kumfukuza mwanafunzi kwa sababu amekosoa utendaji mbaya wa kazi katika chuo kikuu haikubaliki.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.