Pata taarifa kuu
SUDAN

UN yaongeza muda kwa vikosi vyake Darfur

Baraza la usalama la umoja wa Mataifa limekubali kuongeza muda zaidi wa vikosi vyake vya kulinda amani kwenye jimbo la Darfur nchini Sudan, baada ya kupokea mapendekezo kutoka kwa Serikali mpya ya mpito.

RFI/ Abuso
Matangazo ya kibiashara

Tume ya kulinda amani kwenye jimbo la Darfur inayofahamika kama UNAMID, iko chini ya usimamizi wa umoja wa Afrika na umoja wa Mataifa ambao kwa pamoja juma hili wamepiga kura kuunga mkono azimio la kuongezwa muda zaidi kwa wanajeshi wake kusalia nchini humo.

Vikosi hivyo vilikuwa vimalize muda wake mwezi Juni mwaka huu lakini viliongezewa miezi minne zaidi baada ya kutokea maandamano yaliyosababisha kuondolewa madarakani kwa rais wa zamani Omar al-Bashir.

Wataalamu wa masuala ya usalama wanaona kuwa amani ya kweli katika nchi ya Sudan Kaskazini italetwa na wasudan wenyewe kwa sababu wao ndio walianza vuguvugu la kutaka kuleta mabadiliko nchini humo na kazi ya Umoja wa Mataifa itakuwa ni kushughulikia masula ya kibinadamu amebainisha Dokta Francis Onditi mtaalamu wa masuala ya usalama kutoka Mairobi nchini Kenya wakati alipozungumza na rfikiswahili.
 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.