Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Mali: Waalimu sita waliotekwa nyara waachiliwa huru

Walimu sita kati ya saba waliotekwa nyara na kundi la watu wenye silaha katika wilaya ya Mopti, katikati mwa Mali wameachiliwa huru. Waalimu hao walitekwa nyara Ijumaa wiki iliyopita na watu wenye silaha wasiojulikana katika mji wa Korientzé, wilayani Mopti katikati mwa Mali.

Mwanafunzi akiwa shuleni, Gao, Mali, Aprili 12, 2013. (Picha ya kumbukumbu)
Mwanafunzi akiwa shuleni, Gao, Mali, Aprili 12, 2013. (Picha ya kumbukumbu) © AFP/Joel Saget
Matangazo ya kibiashara

Taarifa hiyo imethibitishwa na serikali ya Mali. Waalimu sita waliotekwa nyara siku ya Ijumaa katika shule yao katikati mwa Mali na wanajihadi wameachiliwa huru, serikali imesema, bila kueleza mazingira ya kuachiliwa kwao.

"Serikali ya Jamhuri ya Mali inatangazia umaa na ulimwengu kuhusu kuachiliwa huru kwa waalimu waliotekwa nyara siku ya Ijumaa Oktoba 25, 2019, wakati wa shambulio katika shule moja inayopatikana katika mji wa Korientzé, shambulio lililoendeshwa na watu wenye silaha," serikali imesema katika taarifa.

"Serikali inakaribisha nia njema ya wale wote waliochangia kwa kuachiliwa huru kwa waalimu hao," serikali imeongeza, bila maelezo zaidi.

Mmoja wa waalimu saba waliotekwa nyara bado yuko mikononi mwa watekaji nyara, kwa mujibu wa Abdul-Wahad Diallo, katibu mkuu wa chama cha waalimu wa shule za msingi wilayani Mopti. Akihojiwa na RFI, Bw Diallo amekumbusha kwamba shule tatu zilishambuliwa kwa siku moja.

Abdul-Wahad Diallo amebaini kwamba watekaji nyara wanadai kwamba hawataki shule za Ufaransa.

"Kwa kweli serikali inawajibika kutoa ulinzi wa kutosha katika shule< " amesema Abdul-Wahad Diallo, katibu mkuu wa chama cha waalimu wa shule za msingi wilayani Mopti.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.