Pata taarifa kuu
DRC-KATUMBI-SIASA

Katumbi awaacha vinywa wazi wakaazi wa Goma

Wakaazi wa Goma na viunga vyake wanaendelea kuhoji kauli ya hivi karibuni ya mwanasiasa wa upinzani Moise Katumbi Chapwe aliyerejea hivi karibuni nchini DRC kutoka uhamishoni, baada ya kubaini kwamba hashirikiani na muungano wa Joseph Kabila Kabange.

Mwanasiasa wa upinzani nchini DRC, Moise Katumbi, baada ya miaka mitatu akiwa uhamishoni, Mei 20, 2019.
Mwanasiasa wa upinzani nchini DRC, Moise Katumbi, baada ya miaka mitatu akiwa uhamishoni, Mei 20, 2019. Junior KANNAH / AFP
Matangazo ya kibiashara

Jumamosi ya wiki hii iliyopita Moise Katumbi aliwasili Goma, baada ya ziara yake hiyo kusitishwa mara mbili.

Bw Katumbi alifanya mkutano katika uwanja wa Afia ambapo alikanusha ushirikiano wowote na muungano wa Joseph Kabila.

Mbele ya umati mkubwa wa watu waliokuja kumlaki kwenye uwanja wa ndege hadi uwanja wa Afia, Moise Katumbi kwanza alionyesha furaha yake kuona amewasili Goma:

"Tulikosa fursa kadhaa za kuonana tena, ninaelewa kwa kuona umati huu wa watu. Ninakaribisha mwenendo huu wa kimapinduzi kwa sababu niko hapa kwa ajili yenu ".

Katumbi aliahidi kufanya upinzani wenye ushawishi mkubwa kupitia chama chake mwenyewe cha siasa anachotaka kuunda. Kuhusu madai ya uhusiano kati yake na rais wa zamani Joseph Kabila, alijibu: "Huu ni upuuzi mtupu. Msitegei sikio maneno haya hata kidogo. Siwezi kusaliti raia. Tunafahamiana! Kama ningekuwa msaliti, je ningeweza kuja hapa? Acheni kusikilia uzushi. "

Moise Katumbi pia alitoa wito wa kupambana dhidi ya ufisadi na utawala mbaya na kuahidi kupigania ustawi wa jamii ya watu wa DRC.

Hata hivyo wakaazi wengi wa mji wa Goma na viunga vyake wameendelea kuhoji kauli hii ya Katumbi, miezi michache baada ya kurejea nchini kutoka uhamishoni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.