Pata taarifa kuu
DRC-MINEMBWE-USALAMA

Jeshi la DRC laonya makundi ya kikabila yanayopigana Minembwe

Jeshi la DRC limeyataka makundi yanayopigana katika eneo la Minembwe, Fizi na katika bonde la Ruzizi kukubali kuweka silaha chini, kauli ambayo imetolewa wakati huu juhudi za kuyapatanisha makabila yanayozozana kwenye maeneo hayo zikiendelea.

Kambi ya walinda amani kutoka Pakistani katikati mwa eneo la Minembwe, Oktoba 21, 2019.
Kambi ya walinda amani kutoka Pakistani katikati mwa eneo la Minembwe, Oktoba 21, 2019. Sonia Rolley/RFI
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza na RFI Idhaa ya Kifaransa, msemaji wa Jeshi hilo katika Operesheni Sokola2 katika mkoa wa Kivu Kusini Dieudonnee Kasereka amefahamisha kuwa jeshi limeimarisha usalama kwenye miji na vijiji kadhaa katika maeneo ya Fizi na Uvira, akitupilia mbali tuhuma kwamba jeshi limekuwa likitetea kabila moja.

Mapema wiki hii tume ya Umoja Mataifa nchini DRC, MONUSCO, ilipendekeza kuanzishwa kwa operesheni ya kuwapokonya silaha wapiganaji wanaowakilisha makabila yao katika eneo hilo.

Kauli hii imetolewa wakati huu hali ya usalama imeendelea kuzorota katika eneo hilo ambako mamia kwa maelfu ya wakaazi wamelazimika kuyatoroka makazi yao kufuatia mapigano kati ya makundi ya mai mai na wapiganaji wengine wenye silaha katika eneo la Minembwe.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.