Pata taarifa kuu

Wananchi wa Botswana wanapiga kura kumchagua rais mpya

Wananchi wa Bostwana wanapiga kura leo, katika Uchaguzi ambao unaelezwa kuwa unaleta ushindani mkubwa kwa chama tawala cha BDP ambacho kimekuwa madarakani kwa muda mrefu.

Kuanzia kushoto kwenda kulia Duma Boko wa UDC, Biggie Butale wa BDF, Rais Mkgweetsi Masisi (mgombea wa chama cha BDP) na Ndaba Gaolathe wa chama cha AP katika mjadala wa televisheni, Gaberone, 16 Oktoba 2019.
Kuanzia kushoto kwenda kulia Duma Boko wa UDC, Biggie Butale wa BDF, Rais Mkgweetsi Masisi (mgombea wa chama cha BDP) na Ndaba Gaolathe wa chama cha AP katika mjadala wa televisheni, Gaberone, 16 Oktoba 2019. Thalefang Charles /www.mmegi.bw
Matangazo ya kibiashara

Chama cha Botswana Democratic Party (BDP) kinakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka muungano wa upinzani Umbrella for Democratic Change (UDC), ambao unapewa nafasi kubwa ya kushinda.

Kiongozi mkuu wa upinzani na kiongozi muungano wa upinzani Umbrella for Democratic Change (UDC) Duma Boko, anatarajiwa kuleta ushindani mkali kwa rais wa sasa anayetetea kiti chake Mokgweetsi Masisi.

Boko anaungwa mkono na rais wa zamani Ian Khama, suala ambalo limemwongezea nguvu kuelekea katika Uchaguzi huu.

Jeshi limekataa kutumiwa kama hoja ya uchaguzi, wakati wa kampeni ya uchaguzi yenye ushindani mkubwa nchini Botswana, huku kila upande ukinadi sera yake kwa wafuasi wake.

Mapema wiki hii mgombea wa muungano wa upinzani, Umbrella for Democratic Change (UDC), alirusha picha za askari kwenye mitandao ya kijamii, ambao amejaribu kutetea mazingira yao ya kazi. Lakini, sheria inabaini kuwa jeshi halina upande wowote linaloegemea katika siasa. Jeshi limekanusha taarifa kutoka upinzani kwamba, linaegemea upande wa chama tawala, kwa kuwa jeshi linamsafirisha rais anayemaliza muda wake katika ndege zake katika maeneo mbalimbali ya nchi.

Kwa upande wake, Rais Mkgweetsi Masisi mwenye umri wa miaka 58, mtoto wa waziri, mwigizaji wa zamani na mwalimu wa shule ya upili, amesema ana imani kuwa Chama chake cha Botswana Democratic Party (BDP), madarakani tangu Botswana kupata Uhuru mwaka 1966 kitashinda uchaguzi huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.