Pata taarifa kuu
RWANDA-CAR-USHIRIKIANO

Ziara ya Kagame Bangui: Touadéra ataka kuiga mfano wa Rwanda

Rwanda na Jamhuri ya Afrika ya Kati zimetia zaini mikataba mitano ya kijeshi na uchumi kwa lengo la kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili. Rais wa Rwanda ambaye amezuru Jamhuri ya Afrika ya Kati jana Jumanne alipokelewa na mwenyeji wake Rais Touadéra.

Rais wa Rwanda Paul Kagame (kulia) na mwenyeji wake, Faustin Archange Touadéra (kushoto), katika Ikulu ya Rais (Palais de la Renaissance) Bangui, Oktoba 15, 2019.
Rais wa Rwanda Paul Kagame (kulia) na mwenyeji wake, Faustin Archange Touadéra (kushoto), katika Ikulu ya Rais (Palais de la Renaissance) Bangui, Oktoba 15, 2019. © Gaël Grilhot/RFI
Matangazo ya kibiashara

Hii ni ziara ya kwanza ya rais kutoka nchi ya Afrika kufanya nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Mikataba ya kijeshi na kiuchumi pamoja na madini na mafuta, imesainiwa. Haya ni matokeo ya mazungumzo ya marais hao wawili wakati wa maadhimisho ya miaka 25 ya ukombozi wa Rwanda mwezi Julai jijini Kigali.

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra amesema anataka kuiga mfano wa Rwanda katika kuleta maendeleo endelevu nchini mwake.

"Natumai kwamba uhusiano wetu wa nchi hizi mbili utakuwa mfano wa ushirikiano wa kanda ya Kusini ambao utakuwa chini ya maadili muhimu ya mshikamano, ushirikiano, na kuingiliana katika masuala mbalimbali kwa lengo la kuimarisha historia ya nchi hizi mbili," Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra amesema. "Jamhuri ya Afrika ya Kati inataka kuiga mfano na ujuzi kutoka Rwanda kwa lengo la kujenga taifa lenye nguvu, umoja na mafanikio," ameongeza.

Kwa upande wa Rais wa Rwanda, amesema njia ya kuondokana na mzozo ni kupitia mazungumzo na makubaliano.

"Kwa upande wa Rwanda, mchakato wa kutunza amani umekuwa dhamira thabiti kwa umoja wa kitaifa, " amesema Rais Paul Kagame.

Hatua kubwa inayofuata ni uundwaji wa tume ya pamoja kwa nchi zote mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.