Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 19/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Habari mpya kabisa
Afrika

Maswali mengi yaibuka kuhusu ajali ya ndege ya serikali DRC

media Ndege ya mizigo aina ya Antonov yenye chapa AN-72. Aina ya ndege jeshi la DRC iliyotumiwa na ofisi ya rais kwa kusafirisha gari na walinzi wa rais Tshisekedi ambayo ilianguka Oktoba 10, 2019. (Picha ya kumbukumbu) © Creative Commons Flickr CC BY-SA 2.0 Lars Plougmann

Rais wa DRC Felix Tshisekedi Tshilombo amekutana na familia ya waathiriwa wa ajali ya ndege ya serikali Antonov 72. Dereva wake na maafisa wake kadhaa wa ulinzi walikuwa katika ndege hiyo.

Ofisi ya rais ilithibitisha rasmi Jumanne wiki hii kuwa mabaki ya ndege hiyo yamepatikana katika eneo la Sankuru na kuahidi kufanya kilio chini ya uwezo wake ili ukweli kuhusu mazingira ya ajali hiyo ujulikane.

Miili ya kwanza iliyopatikana karibu na mabaki hayo yamesafirishwa na kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini DRC, MONUSCO.

Mamlaka imethibitisha kuwa miili ya watu wanne imepatikana, huku rubani amethibitishwa kupatikana akiwa hai.

Maswali yameibuka kuhusu ajali ya ndege hiyo ya jeshi la DRC, ambayo ilikuwa imetumiwa na ofisi ya rais kwa kusafirisha gari ya rais na walinzi wake wa karibu Mashariki mwa DRC.

Ndege hiyo ilipotea siku ya Alhamisi ikiwa na watu watano, mmoja wapo akiwa dereva maalumu wa rais Tshisekedi.

Awali palikua na taarifa kinzani kuhusu mahali ndege hiyo ilipo pamoja na idadi ya watu waliokuwemo.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana