Pata taarifa kuu
AFRIKA KUSINI-ZUMA-HAKI

Afrika Kusini: Kesi ya Jacob Zuma yaahirishwa kwa mara nyingine

Kesi ya ufisadi ya Jacob Zuma iliyotarajiwa kusikilizwqa Jumanne wiki hii imeahirishwa tena. Rais huyo wa zamani anatuhumiwa kupokea rushwa kutoka kwa kampuni ya Ufaransa ya Thales katika miaka ya 1990.

Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma akiondoka katika Mahakam Kuu ya Pietermaritzburg baada ya kesi yake kuahirishwa tena, Oktoba 15, 2019.
Rais wa zamani wa Afrika Kusini Jacob Zuma akiondoka katika Mahakam Kuu ya Pietermaritzburg baada ya kesi yake kuahirishwa tena, Oktoba 15, 2019. © REUTERS/Rogan Ward
Matangazo ya kibiashara

Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Jacob Zuma, anaandelea kukabiliwa na kashfa mbalimbali ikiwa ni pamoja na ufisadi, kashfa ambazo zilisababisha kung'atuliwa madarakani mwaka 2018.

Kesi yake inahusiana na rushwa katika kesi ya zamani, miaka ishirini iliyopita, ya mkataba wa silaha, kesi ambayo inaihusisha kampuni ya Ufaransa Thales.

Jacob Zuma, aliyekaa madarakani kuanzia mwaka 2009 hadi mwaka 2018, anashitakiwa kwa kosa la ufisadi, utakatishaji wa fedha na kupitisha mlango wa nyuma pesa kuhusu mkataba mkubwa wa silaha wa Randi bilioni 51 (sawa na Euro bilioni tatu kwa bei ya sasa) mkataba uliotolewa mwaka 1999.

Wakati wa mashtaka dhidi yake, alikuwa "waziri" katika ngazi ya mkoa na baadaye makamu wa rais. Anatuhumiwa kuwa alipokea Randi milioni 4 ( sawa na Euro 249,000 kwa bei ya sasa) kama hongo kutoka kampuni ya Ufaransa ya Thales.

Jacob Zuma na kampuni hiyo inayotengeneza vifaa vya kielektroniki na ulinzi, ambayo pia inakabiliwa na mashitaka hayo, wameendelea kukana mashitaka dhidi yao.

Baada ya kesi hiyo kusheleweshwa kwa miaka kumi na tano, Mahakama, siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita iliamua kuruhusu kesi hiyo inayomkabili rais wa zamani wa Afrika Kusini kuanza kusikilizwa kwa undani, baada ya kufutilia mbali ombi la Jacob Zuma la kuachana na mashtaka dhidi yake.

Kesi hiyo ambayo ilitarajiwa kuanza leo Jumanne katika Mahakama Kuu ya Pietermaritzburg, Mashariki mwa Afrika Kusini, imeahirishwa tena.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.