Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 21/11 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 20/11 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Mazungumzo ya amani kuanza tena Sudani Kusini

media Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok anatarajia kushiriki mazungumzo ya amani na waasi kutoka Majimbo ya Darfur, Kordofan Kusini na Blue Nile mazungumzo ambayo yanaanza tena Jumatatu Oktoba 14 jijini Juba. © REUTERS/Mohamed Nureldin Abdallah

Mazungumzo ya amani kati ya Khartoum na waasi wa majimbo ya Sudani ya Darfur (magharibi), Kordofan Kusini (kusini) na Blue Nile (kusini-mashariki) yanatarajiwa kuanza tena leo Jumatatu katika mji mkuu wa Sudan Kusini mbele ya Waziri mkuu wa Sudan, Abdallah Hamdok.

Mazungumzo ya amani nchini Sudan yanaanza Jumatatu hii (Oktoba 14) katika mji mkuu wa Sudani Kusini, Juba, na yanatarajiwa kudumu mwezi mmoja, kulingana na kile kilichofikiwa kwenye mkataba wa Septemba 11 kati ya serikali ya mpito na makundi yenye silaha.

Ni mazungumzo ya moja kwa moja lakini ya wazi na makundi mawili makubwa yenye silaha.

Sudan imejipa miezi sita kufikia mkataba kamili. Kupata amani ya kudumu nchini Sudani ni kipaumbele cha serikali ya mpito, kama alivyobaini mara kadhaa Waziri Mkuu Abdalla Hamdok. Kwa hivyo hii ni hatua ya kwanza katika mazungumzo ambayo yanapaswa kufikia amani kamili ya kudumu nchini Sudani.

Viongozi wengine wakiwemo Waziri Mkuu wa Ethiopia Abiy Ahmed, rais Kenya Uhuru Kenyatta na mwenzake wa Uganda Yoweri Museveni, wanatarajiwa pia kuhudhuria.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana