Pata taarifa kuu
SOMALIA-MAREKANI-USHIRIKIANO

Ubalozi wa Marekani nchini Somalia wafunguliwa tena

Hatua hii ya Marekani kufungua tena ubalozi wake Mogadishu ni ishara tosha na kubwa, karibu miongo mitatu baada ya ubalozi huo, ulioko katika eneo la uwanja wa ndege wa kimataifa, kufungwa. "Hii ni hatua mpya kuelekea kurudi kwa uhusiano kati ya Somalia na Marekani," Washington imesema katika taarifa.

Picha isiyo na tarehe ya ubalozi wa zamani wa Marekani mjini Mogadiscio.
Picha isiyo na tarehe ya ubalozi wa zamani wa Marekani mjini Mogadiscio. © DR.
Matangazo ya kibiashara

Mnamo tarehe 5 Januari 1991, wakati Somalia ilitumbukia katika vita vya wenyewe kwa wenyewe, watu 281 walihamishwa kutoka ubalozi wa Marekani hadi kwenye chombo cha jeshi la Marekani kilokuwa kimepiga kambi kwenye pwani ya Mogadishu.

Imechukua miaka 28 kwa Marekani kufungua tena uwakilishi wao katika mji mkuu, wa Somalia, Mogadishu. Kitendo chenye ishara kubwa, kuonyesha jinsi gani usalama umeimarika nchini Somalia na nchi hizi mbili kuanza tena ushirikiano mpya.

Wakati huo huo, Washington ilitambua serikali ya Somalia mnamo mwaka 2013, miaka miwili baada wanamgambo wa Kiislamu, Al Shabab, kuondoka katika mji wa Mogadishu.

Hatua hii ya kufunguliwa tena kwa ubalozi wa Marekani nchini Somalia inakuja miaka mitano baada ya uteuzi wa balozi

Mwezi Februari 2015, rais Barak Obama aliteua balozi wa kwanza wa Marekani nchini Somalia tangu kuzuka kwa vita na miezi mitatu baadaye, wizara ya mashauriano ya kigeni ilitangaza kufungua tena ubalozi katika mji mkuu wa nci hiyo Mogadishu. Imechukua karibu miaka 5 ili ubalozi huo ufunguliwe tena katika mji huo.

Balozi wa sasa wa Marekani Nchini Somalia, Donald Yamamoto ameelezea kufunguliwa kwa ubalozi huo Jumatano wiki hii kuwa ni "siku ya kihistoria inayoonyesha maendeleo ya Somalia katika miaka ya hivi karibuni. Ubalozi huo utasaidia kuimarisha ushirikiano na kuendeleza masilahi ya kimkakati ya Marekani. "

Msaada mpya wa dola milioni 257 watolewa kwa Somalia

Leo, Marekani ndiye mfadhili mkubwa zaidi nchini Somalia. Jumatano wiki hii, Mareani imetangaza kutoa msaada mpya wa dola milioni 257 kwa Somalia.

Marekani pia inaona Somalia kama eneo la kimkakati. Kambi maalumu ambazo zitakuwa na operesheni za kupambana na ugaidi zimejengwa, na zinaendelea kuwa kupanuliwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.