Pata taarifa kuu
NIGERIA_AFRIKA KUSINI-USHIRIKIANO

Rais wa Nigeria aanza ziara ya kiserikali Afrika Kusini katika hali tete

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa anampokea leo Alhamisi (Oktoba 3) mwenzake wa Nigeria Muhammadu Buhari. Ziara hii iliyopangwa kwa muda mrefu inakuja wakati huu uhusiano wa nchi hizi mbili umeingiliwa na dosari kufutia chuki dhidi ya ubaguzi wa rangi iliyokuwa ikiendelea nchini Afrika Kusini.

Muhammadu Buhari, Rais wa Nigeria mwishoni mwa mwezi Septemba katika Mkutano Mkuu wa 74 wa Umoja wa Mataifa, New York.
Muhammadu Buhari, Rais wa Nigeria mwishoni mwa mwezi Septemba katika Mkutano Mkuu wa 74 wa Umoja wa Mataifa, New York. © REUTERS/Carlo Allegr
Matangazo ya kibiashara

Mwezi mmoja uliopita, raia kadhaa wa kigeni waliuawa kikatili na baadhi ya wananchi wa Afrika Kusini. Kisa ambacho kililaniwa na mataifa mengi duniani hasa nchi za Afrika.

Karibu maelfu ya raia wa Nigeria waliokuwa wakiishi nchini Afrika Kusini waliamua kutoroka na kukimbilia nchi jirani na wengine walilazimika kurejea nchini mwao.

Hakuna kiongozi kutoka Nigeria aliyefanya ziara rasmi nchini Afrika Kusini tangu miaka sita iliyopita. Kwa mujibu wa Peter Fabricius wa Taasisi inayotathmini masuala ya Usalama jijini Pretoria, "uhusiano kati ya marais hao wawili sio mbaya, lakini hata hivyo uhusiano kati ya nchi zao, sio mzuri kabisa.

"Nchi hizi mbili zilizostawi kiuchumi barani Afrika zina uhusiano unaokabiliwa na ukinzani fulani. Miezi miwili iliyopita, ziara hii ilitangazwa kwanza kama ziara yenye lengo la kuimarisha uchumi kati ya nchi izo mbili, fursa kwa nchi zote mbili kuimarisha uhusiano wao wa kibiashara.

Ikulu ya rais jijini Abuja, inasema, rais Buhari na mwenyeji wake rais , Cyril Ramaphosa watajadili usalama wa raia wa Nigeria nchini Afrika Kusini.

Serikali ya Nigeria inaamini kuwa, maeneo ya biashara ya raia wake yameendelea kulengwa suala ambalo limesababisba mamia ya raia wkae kurejea nyumbani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.