Kusikiliza Pakua Podcast
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 04h30 - 05h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 04h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 05h30 - 06h00 TU
    Uchambuzi na makala 18/01 05h30 GMT
  • Sikiliza taarifa za habari zilizopita 15h00 - 16h00 TU
    Uchambuzi na makala 17/01 15h00 GMT
Ili Kufurahia kikamilifu maudhui ya multimedia yetu, unahitaji kuwa na Plugin iliyowekwa kwenye kompyuta yako Ili kuingia, unahitaji kuruhusu cookies zote kwa kuseti vizuri Ili kutembelea mtandao, tovuti ya RFI inaenda sambamba na Internet Explorer 8 na + Firefox 10 na +, Safari 3 na +, Chrome 17 na + nk
Afrika

Mgombea urais Tunisia Nabil Karoui asalia jela

media Mfanyabiashara na mmiliki wa kituo cha televisheni cha Nessma TV Nabil Karoui, Agosti 2, 2019. REUTERS/Zoubeir Souissi/File Photo

Mahakama ya Rufaa nchini Tunisia imefutilia mbali ombi la kuachiliwa huru Nabil Karoui lililotolewa na mawakili wake. Nabil Karoui amefuzu katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini humo. Duru ya pili ya uchaguzi wa urais imepangwa kufanyika Oktoba 13 mwaka huu.

Nabil Karoui, ambaye ni mfanyabiashara maarifu nchini Tunisia, ameshitakiwa tangu mwaka 2017 kwa utakatishaji fedha na ukwepaji kodi.

Nabil Karoui hatashiriki katika kampeni ya uchaguzi wa wabunge. Wafuasi wake, pamoja na mkewe, Salwa Smaoui, wataendelea kunadi sera yake katika maeneo mbali mbali ya nchi hiyo, kama walivyofanya tangu mapema mwezi Septemba.

Kuna swali moja ambalo bado halijawekwa wazi: lile la kushiriki kwa mfanyabiashara huyo katika mijadala ya televisheni na mpinzani wake Kaïs Saeid kwa duru ya pili ya uchaguzi wa urais.

Uamuzi huu wa Mahakama ya Rufaa pia unaendelea kuzua wasiwasi kuhusu Nabil Karoui iwapo atashinda uchaguzi. Na uamuzi huo unaonekana kuwa utazua sintofahamu kuhusu uaminifu kwa matokeo ya uchaguzi, wadadisi wamesema.

Katika siku za hivi karibuni, chama chake, wapinzani wa kisiasa, waangalizi wa kimataifa walitoa wito wa kutaka Nabil Karoui aweze kufanya Kampeni kama wagombea wengine, bila mafanikio.

Kuhusu mada hiyo hiyo
 
Samahani, mwunganisho na sava umeshindikana