Pata taarifa kuu
SUDANI-UFARANSA-USHIRIKIANO

Ufaransa yatoa msaada wa kifedha kwa serikali ya mpito Sudani

Ufaransa imekubali kutoka msaada wa kifedha kwa Serikali ya mpito nchini Sudan, baada ya jeshi na viongozi wa maandamano kufikia mkataba wa kihistoria wa kugawana madaraka.

Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok akikutana kwa mazungumzo na Rais wa Ufaransa Emmanuelle Macron. Septemba 30, 2019
Waziri Mkuu wa Sudan Abdallah Hamdok akikutana kwa mazungumzo na Rais wa Ufaransa Emmanuelle Macron. Septemba 30, 2019 © REUTERS/Philippe Wojazer
Matangazo ya kibiashara

"Msaada usio na masharti kwa Serikali ya mpito kwa kuimarisha na kuendeleza kidemokrasia," Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametangaza Jumatatu hii Septemba 30 baada ya kukutana kwa mazungumzo na Waziri Mkuu wa Sudan, Abdallah Hamdok jijini Paris.

"Mapinduzi ya Desemba yalikaribishwa na ulimwengu na bara la Afrika. Ndio maana Ufaransa itaambatana nawe katika hatua hii ya mageuzi ya kihistoria, "ameongeza Rais wa Ufaransa. Msaada huu unaendana haswa na msaada mkubwa wa kifedha.

Ufaransa itatoa msaada wa euro milioni 60, ikiwa ni pamoja na milioni 15 ambazo zitapatikana mapema, amesema Rais Emmanuel Macron. Kwa upande wa Rais wa Ufaransa Ufaransa, amesema ni muhimu mapinduzi ya Sudani yawe mafanikio, na kwa hiyo, suala la kufufua uchumi wa nchi hiyo linapaswa kupewa kipaumbele.

Mgogoro wa kiuchumi ndio uliosababisha mapinduzi hayo ya Desemba mwaka jana.

Sudani kuondolewa kwenye orodha ya nchi zinazounga mkono ugaidi

Rais wa Ufaransa pia ametangaza kuwa kutafanyika mkutano wa kimataifa wa wafadhili utakaofanyika jijini Paris. Hakuweza kutangaza tarehe. Hii itategemea kufutwa kwa vikwazo dhidi ya Khartoum.

Ufaransa imeahidi kuendelea kutetea kwa Marekani kuindoa Sudani kwenye orodha ya nchi zinazofadhili au kuunga mkono ugaidi.

Waziri Mkuu wa Sudani Abdallah Hamdok alimshukuru Emmanuel Macron kwa msaada wake kwenye suala hilo. "Raia wangu hawajawahi kuunga mkono ugaidi. Ugaidi uliuungwa mkono na utawala wa zamani. Sisi ni watu wa amani", amesema Bw Hamdok.

Kuondolewa kwenye orodha hii "itakuwa ufunguo wa kutatua shida zetu zingine: kukopa, amani, uwekezaji na Sudani kuweza kuwekeza nje," ameongeza Waziri Mkuu ambaye ametoa wito kwa makampuni ya Ufaransa kuja kuwekeza nchini Sudani. "Mnakaribishwa tena nchini Sudani, kutokuwepo kwenu kumechukua muda mrefu sana na ni wakati wa nyinyi kurudi kufanya kazi pamoja ili kujenga nchi hii nzuri," amesema Bw Hamdok.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.