Mugabe sasa kuzikwa katika kijiji alichozaliwa
Rais wa zamani wa Zimbabwe sasa atazikwa katika kijiji alichozaliwa katika eneo la Zvimba,, hii ikiwa ni awamu nyingine ya mvutano kati ya familia na serikali ni wapi kiongozi huyo azikwe.
Imechapishwa:
Awali, serikali ilikuwa imesema Mugabe aliyefariki dunia mapema mwezi Septemba akiwa na umri wa miaka 95 akiwa nchini Singapore, angezikwa katika makaburi ya mashujaa jijini Harare.
Uamuzi wa serikali ulikubaliwa na Familia, lakini hilo limebadilika na haijawa wazi ni kwanini serikali ya Zimbabwe imefanya mabadiliko haya.
Hata hivyo, Waziri wa Habari nchini humo Nick Mangwana katika taarifa yake amesema, serikali imeona ni vema itii matamanio ya familia kuhusu ni wapi mpendwa wao azikwe.
Mwezi huu kulikuwa na ibada ya kumbumbuka Mugabe iliyofanyika jijini Harare na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali kutoka barani Afrika.